Mwalimu Kiongozi wa huduma ya matengenezo ya kiroho Augustine Tengwa ameviomba vyama vya siasa nchini kutogombania madaraka kuilinda amani ya Tanzania


Ametoa kauli hiyo Octoba 11 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maono

ambayo watumishi wamefunuliwa kuelekea uchaguzi kuwa kutakuwa na umwagikaji damu ya mauaji ya wenyewe kwa wenyewe.


“Tuilinde amani tuliyonayo hatujawahi kuwa wakimbizi kama mataifa mengine ya jiran tusije kuwakama Rwanda, Kenya, Libya, Ukraine na Israel na hamas”


Kwa upande wake Nabii Alpha Kiamba amewaasa Watanzania kutopuuza taarifa kutoka kwa watumishi wa Mungu hasa maono bali kuyapokea na kufanyia maombi


Akitolea mfano maporomoko ya mlima hangang na mafuriko ya rufiji amesema hayo yalikuwa maono kutoka kwa watumishi na hilo la uchaguzi lisipuuzwe


Nae, Mtumishi Agness Bruno amewaasa Watanzania kurudi kuwa taifa moja na wamoja kwa kujua thamani ya kila Mtanzania ili kuepusha umwagaji damu.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...