▫️Kanenda dhidi ya Amroug El Abidine kutoka Morocco
21-10-2024, Kinshasa - DR Congo: Mabondia wa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ngumi "Faru Weusi" Zulfa Macho na Saidi Hamisi Kanenda wanatarijiwa kupanda ulingoni leo katika mashindano ya AFBC Ubingwa wa Afrika - Kinshasa 2024 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Zulfa atapanda ulingoni katika session ya 4 majira ya alasiri (muda wa Kinshasa Gmt +1) dhidi ya mpinzani wake Bisambu Merveille, mwenyeji wa DR Congo katika uzani wa Bantamweight 54kg.
Saidi Kanenda naye atapanda ulingoni usiku wa leo katika session ya 5 uzani wa Light middleweight 71kg dhidi ya Amroug El Abidine kutoka Morocco.
Mashindano haya yameanza rasmi tarehe 18-10-2024 na yatafikia tamati kwa fainali kuchezwa siku ya Jumamosi 26-10-2024.
Tanzania inawakilishwa na mabondia watatu (3) ambao ni Saidi Kanenda (Light middleweight 71kg), Zulfa Macho (Bantam 54kg) na Najma Isike (Light welterweight 63kg) huku wakisimamiwa na Mwalimu Mkuu IBA 1 Star Samwel Kapungu.
"Mungu wabariki Zulfa na Kanenda, Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿"
✍🏽 Ofisi ya Rais - BFT
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...