Na Mwandishi wetu, Simanjiro
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, kimewapongeza wasimamizi wa uchaguzi kwa kutenda haki na kuwapitisha wagombea uenyekiti wa vitongoji na vijiji bila kukata majina yao.
Katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Simanjiro Ambrose Ndege ameeeleza kuwa wanatarajia kuanza kufanya kampeni ya uchaguzi November 20 kwenye maeneo mbalimbali.
"Tunawashukuru viongozi wa Wilaya Simanjiro na kata zote na za kata za mji mdogo wa Mirerani kwa kutenda haki bila kubagua au kukata majina ya wagombea wetu," amesema Ndege .
Amesema anaishukuru TAMISEMI kwa kuweka viongozi makini Wilaya ya Simanjiro, kata zote na mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani kwani wamesimamia mchakato wa uchaguzi vyema na sasa wanasubiria kuanza kampeni muda utakapofika.
"Wagombea wote kwenye maeneo tuliyowasimamisha wamepitishwa hakukuwa na vikwazo vya fomu kukosewa au mizengwe yoyote timetendewa haki watu waingie uwanjani wanadi sera zao wapigiwe kura na siyo kupita bila kupingwa," amesema Ndege.
"Tangu mwaka 2014 hatujafanya uchaguzi wa halali Simanjiro kwani wagombea wetu wamekuwa wakienguliwa ila mwaka huu wa 2024 tunawapongeza viongozi wa Serikali kwa kutekeleza vyema wajibu wao," amesema Ndege.
Amesema kwenye mji mdogo wa Mirerani wamefanikiwa kusimamisha wagombea uenyekiti kwenye vitongoji 23 kasoro kitongoji kimoja.
"Huyu mgombea wa Zaire ameandika barua mwenyewe ya kutogombea ila hakukatwa jina lake ameamua mwenyewe hatufahamu kilichomsibu," amesema Ndege.
Mwanachama wa CHADEMA Adam Woiso amesema wasimamizi wa uchaguzi wamefanya vyema kwani jamii inapaswa kufanya uchaguzi kwa kuchagua wagombea kupitia vyama na siyo kuwapitisha bila kupingwa.
"Kwa hapa wasimamizi wa uchaguzi wanastahili pongezi kwani wametekeleza wajibu wao ipasavyo na sisi tunajipanga vyema kwenye maandalizi ya kufanya kampeni," amesema Woiso.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...