Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mcha Hassan Mcha ameipongeza Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kuandaa mafunzo ya siku tatu kwa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuhusu  mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 na kanuni zake za mwaka 2024 pamoja  na usimamizi wa mikataba ya Ununuzi na Ugavi.


Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Naibu Kamishana Mcha amesema PSPTB imefanya jambo muhimu la kutoa mafunzo hayo kwasababu suala la Ununuzi linajumuisha idara mbalimbali katika Mamlaka hiyo hivyo mafunzo hayo yataweza kuwajengea uwezo wataalamu ili wakiwa wanafanya majukumu yao waweze kuyatekeleza kwa ufanisi mkubwa.

 "Mafunzo hayo ni muhimu kwa TRA kutokana na changamoto mbalimbali katika masuala ya Ununuzi na Ugavi." alisema Mcha.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma (PSPTB) Bw. Amos Kazinza  aliyemwakilisha  Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi ameshukuru Mamlaka hiyo kwa kuendelea kuiamini PSPTB katika kuwajengea uwezo watumishi wa TRA.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mcha Hassan Mcha akizungumza na viongozi wa Mamlaka hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Ununuzi na Ugavi yanayotolwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yanayoendelea  jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma wa PSPTB Amos Kazinza akiwasilisha mada kwa viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada mbalimbali wakati wa mafunzo yanayotolewa na PSPTB.
Baadhi ya wasilisha mada kutoka PSPTB wakifuatilia ufunguzi wa Mafunzo kwa viongozi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanywa na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha.
Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha (katikati waliokaa)  akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa TRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...