TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) inatarajia kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ifikapo Mwezi Mei 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba ameeleza hilo katika hafla ya uzinduzi wa usambazaji wa vitabu vya washindi wa tuzo ya Taifa ya Uandishi Bunifu iliyofanyika Novemba 18,2024 katika ofisi za TET Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Komba alisema kuwa, katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50, TET inatarajia kufanya shughuli mbalimbali za kielimu pamoja na za kijamii ikiwemo Kongamano la elimu na matembezi ya hisani.
"Kuelekea miaka hamsini tumejipanga kufanya shughuli kadhaa ambazo zitahusisha kazi zetu katika jamii " alisema Dkt.Komba .
Alisema, tukio hilo litawajumuisha wadau wa Elimu nchini watakaojadili masuala ya Elimu, mafunzo ya walimu kazini, upandaji wa miti kwa ajili ya kutunza mazingira pamoja na matembezi ya hisani ili kupata pesa za kuandaa vitabu kwaajili ya wanafunzi viziwi.
Aidha Dkt. Komba, aliomba wadau wa elimu kuwaunga mkono katika kuelekea kilele cha miaka 50 ya TET.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...