Na Mwandishi Wetu

Shule ya DYCCC Yemen imesema kuwa malezi ya shule kwa kushirikiana na wazazi kunafanya watoto kuwa na muongozo bora wa kufanya vizuri katika elimu.

Hayo aliysesema Mgeni Rasmi na Mwenyekiti wa Bodi wa DYCCC Yemen Sheikh Fawzi Abood katika Mahafali ya Shule ya Awali ya DYCCC Yemen yalitinyika katika viwanja vya Shule hiyo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Shule hiyo hadi kufikia mahafali imefanya kazi kubwa katika kufundisha na kuonyesha wataanza darasa la kwanza wakiwa na msingi mzuri kutokana na kufanya vizuri katika Masomo yao.

"Nimefarijika kuona uwezo wahitimu na kuona mwanga wao utakuwa mzuri hapo baadaye kwani wameonysha wampepikwa na walimu wennye uwezo katika Shule hii"Amesema Abood

Meneja wa Shule Jamila Awadh amesema kuwa shule za DYCCC zinafanya vizuri katika Wilaya ya Temeke kwa Msingi na Sekondari.

Amesema kuwa wameweka mikakati katika kuendelea kutoa elimu bora kutokana na kuwa na walimu wenye uwezo unakidhi mahitaji ya wanafunzi.

Mwalimu Mkuu Msaidizi Naima Issa amesema kuwa kazi shule ya DYCCC kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi wa awali ya wayapende na kuleta matokeo chanya katika kuwafundisha.

Amesema wahitimu hao wameshaandikishwa kuanza darasa la kwanza na kuwataka wazazi kuwepeleka watoto wao katika shule za DYCCC Yemen.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za DYCCC Yemen Fawzi Abood akizungumza katika Mahafali ya Shule ya Awali ya DYCCC Yemen jijin Dar es Salaam.
 

Meneja  wa Shule za DYCCC Yemen Jamila Awadh akizungumza kuhusiana  na mahafali na Mikakati walioiweka katika utoaji wa elimu.
Wahitimu wa shule ya awali ya DYCCC Yemen wakiimba kwenye mahafali yao jijini Dar es Salaam.
 

Baadhi ya wahitimu wa shule ya  Awali ya DYCCC Yemen wakiwa na Vyeti vyao vya uhitimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...