Na Beatus Maganja, Mbeya.
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imekutana leo Machi 18, 2025 Jijini Mbeya Kwa ajili ya kuanza kikao chake cha Kawaida cha 30 cha Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko.
Katika kikao cha siku ya Kwanza (Leo) wajumbe wa kamati za Sera, Mipango na Fedha inayoongozwa na Dr. Simon Mduma na kamati ya Ulinzi wa Rasilimali ya Wanyamapori na Uendeshaji na Usimamizi wa Rasilimali watu inayoongozwa na Prof. Jafari Kideghesho wamekutana na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo na ustawi wa Taasisi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...