Na Said Mwishehe, Rungwe
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Wasira, ameiagiza Kampuni ya GDM kuhakikisha inalipa madeni ya wakulima wa kahawa wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ndani ya siku 14, baada ya kupokea malalamiko ya wakulima hao.
katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Machi 18,2025 katika Stendi ya Mji Mdogo Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo wananchi walitoa kilio cha kuicheleweshewa fedha zao Sh.milioni 664 ambazo wameuza mazao yao ya kahawa Kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa wakulima hao wamemueleza Wasira kwamba ucheleweshaji wa malipo umewaathiri kwa kiasi kikubwa, huku wengi wakikosa fedha za kugharamia mahitaji yao na kuendeleza uzalishaji wa chai.
Kutokana na malalamiko hayo ,Makamu Mwenyekiti wa CCM Wasira ametumia nafasi kueleza kuwa serikali inayotokana na Chama hicho haitavumilia ucheleweshwaji wa malipo ya wakulima, huku akitoa onyo kali kwa kampuni hiyo kuhakikisha inatekeleza agizo hilo ndani ya muda uliowekwa.
"Natoa siku 14 kwa mnunuzi wa chai wa GDM kuhakikisha wakulima wote wanalipwa haki yao bila visingizio. Wakulima hawa wamefanya kazi yao na wanapaswa kuheshimiwa kwa kulipwa kwa wakati," alisema Wasira huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...