Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof Kitila Mkumbo amesema kuna haja ya kurekebisha Sera katika sheria za uagizaji wa Magari ili kulinda viwanda vya utengenezaji Magari nchini

Prof Mkumbo ameyasema hayo wakati alipotembelea Kiwanda cha kutengeneza magari nchini cha GF Vehicle Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani

Akiwa ameambatana na viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Waziri Mkumbo alitembelea kiwanda hicho na kujionea namna wanavyounganisha Magari hayo, kuanzia hatua ya mwanzo mpaka linakamilika,huku akishuhudia uzinduzi wa gari ya 3400 tangu kuanzishwa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho , Ezra Mereng aliwasilisha hoja ya maombi kwa serikali ya kubadilishwa kwa sera na sheria za uagizaji wa magari nchini ili kulinda viwanda vya ndani.

Alisema wao kama kampuni wanafanya upanuzi wa kuingia awamu 3, ambayo inategemewa kufanya uwekezaji wa mtaji wa zaidi ya Bilioni 10 na mpaka sasa imeajiri zaidi ya vijana 200 na katika awamu ya 3 wanatarajia kuajiri zaidi ya vijana 300 wa ajira ya moja kwa moja

"Katika awamu hii tunahitaji vitu vingi vipatikane nchini kama Chuma na vifaa vingine, kwa mfano tumeshaanza kununua betri za magari kutoka katika kiwanda kimoja wapo nchini sasa bila kufanyika kwa mabadiliko ya sheria za kulinda viwanda vya ndani ni kazi bure,

Kwa sasa kumekuwa na uagizahji holela wa magari na katika hili Tanzania tunakuwa walaji wa mwisho kwa kuwa magari mengi ni ya Mtumba (used) Pia kukiwa na sharia ya manunuzi na usimamizi kwa miradi mikubwa ya nchi basi lazima magari au vifaa vitakavyotumika vinunuliwe nchini hii itasaidia kuvilinda viwanda vyetu", alimaliza Ezra.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...