MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, kesi dhidi ya wanandugu wawili na mwenzao mmoja wanaodaiwa kumuua kwa kukusudia ndugu yao Regina Chaula na kumtupa kwenye shimo la maji taka ndani ya nyumba yake bado haujakamilika

Ndugu hao ni Mkulima Mkazi wa Bagamoyo Fred Chaula (56), Dereva Bodaboda Mkazi wa Tegeta Bashiri Chaula (39) na mwenzao Denis Mhwaga (16) Mkazi wa Mafinga,Iringa.

Wakili wa serikali Tumaini Mafuru amedai hayo leo Machi 28,2025 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Rahim Mushi ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 3, 2025 washtakiwa wamerudishwa nyumbani.

Katika kesi hiyo washtakiwa kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa la mauaji ya kukusudia kinyume cha kifungu Cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kama ilivyorejewa mwaka 2019.

Inadaiwa, 18,2025 washtakiwa wakiwa eneo la Bahari Beach ndani ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam walimuua kwa makusudi Regina Chaula.

Awali,Fred na Bashiri walikamatwa na Jeshi la Polisi nchini kwa tuhuma za kumuua dada yao Regina wakati akiwa kwenye harakati za kufuatilia kesi zake za madai zilizopo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Dar es Salaam.

Katika taarifa ya Jeshi hilo, ilidai kuwa Januari 18, 2025 askari walifika nyumbani kwa mama huyo na kubomoa shimo la maji take na kukuta mwili wa Regina, baada ya kutilia shaka shimo hilo ambalo lilikuwa limejengewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...