Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa ya maendeleo kipindi cha miaka 4 kwa mageuzi katika sekta mbalimbali na kuimarika kwa mifumo  pamoja na kuanzisha sera bora kwa uwekezaji zinazolenga kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na kimataifa. 

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika Jukwaa la uwekezaji katika uchumi wa buluu lililofanyika katika Makao makuu ya Ofisi za Citibank, London tarehe 8 Aprili 2025 na kuhudhuriwa na Kampuni mbalimbali za uwekezaji za  Uingereza zenye nia ya kuchangamkia fursa za uwekezaji Zanzibar.

Aidha,  Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha  kuwepo kwa  Citibank kuwa mshirika mkuu wa maendeleo Zanzibar kutachochea zaidi uwekezaji katika sekta za  uchumi wa buluu, nishati , pamoja na nyumba na makaazi.

 Halikadhalika,  Rais Dkt.Mwinyi amesema  ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma unalenga kuzifanya bandari  kuwa za kisasa, uanzishwaji wa viwanda vya usindikaji  wa mazao ya baharini.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa upatikanaji wa fedha utaisaidia Serikali kuendelea kuwawezesha Wanawake wakulima wa Mwani, wavuvi  na vijana  katika mafunzo  ya ujuzi mbalimbali.

Kwa upande mwingine,  Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito katika jukwaa hilo  kuwekeza katika sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki, utalii wa mazingira, na uhifadhi wa baharini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...