Na Issa Mwadangala

Askari Polisi wa kike Mkoani Songwe wajidhatiti kuendelea kiuchumi na kuwa na afya bora ya akili na mwili kwa kufanya semina, sherehe na midahalo mbalimbali ili kuendelea kujiimarisha kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa Aprili 22, 2025 na Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Songwe (TPF- Net) Mkoa wa Songwe Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban katika kikao cha mipango mikakati kuelekea kuwaaga wastaafu, kuyafariji makundi yenye uhitaji, kujengewa uelewa kuhusu elimu ya afya ya akili, uzazi na magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kufanya sherehe ya TPF Net Gala inayofanyika kila mwaka.

ACP Akama alisema, wakati wakielekea kwenye sherehe hiyo inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, wamejipanga kupata elimu pamoja na kuwafariji wahitaji katika jamii.

"Jeshi la Polisi hasa Askari wanawake hatuna budi kulifanya hili ili kuendelea kujenga ukaribu kati yetu na jamii kwa lengo la kupata taarifa za uhalifu na kuzishughulikia pindi tuzipatazo na jamii iendelee kuwa salama" alisema ACP Akama.

Katika kikao hicho alielezea umuhimu wa siku hiyo ambayo inalenga kuunga mkono harakati zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kumuwezesha mwanamke kwenye nafasi za uongozi, uchumi na maamuzi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...