Benki ya Taifa ya Biashara (NBC Bank) imeelezea dhamira yake ya kuyatumia Mashindano ya mbio za magari ya Iringa Mkwawa Rally yanayofanyika kila mwaka mkoani Iringa ili kutangaza na kuimarisha sekta ya utalii katika mkoa huo unaosifika kwa utalii wa kiutamaduni na vivutio mbalimbali vya asili.

Dhamira ya benki hiyo imewekwa wazi na Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC Bw Abel Kaseko wakati akizungumza kwenye hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo msimu wa mwaka 2025 yaliyofanyika kwa siku mbili mwishoni mwa wiki mkoani Iringa yakifahamika kama NBC Iringa Mkwawa Rally 2025 . Benki ya NBC ilikuwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo yaliyovutia washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.

 

Kwa mujibu wa Bw Kaseko, benki hiyo imejipanga kutumia mashindano hayo kama namna ya kuchochea kasi ya ukuaji wa utalii wa ndani katika mkoa wa Iringa kutokana na ushawishi mkubwa wa mchezo huo katika kuwavutia watazamaji na washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.

 

"Tumejizatiti kutumia jukwaa hili la NBC Iringa Mkwawa Rally kuonyesha vivutio vingi vya utalii vilivyopo katika eneo hili, ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo ndio hifadhi kubwa zaidi nchini Tanzania pamoja na vivutio vingine vingi vya kihistoria na kiutamaduni" Kaseko alifafanua.

 

Kwa mujibu wa Bw Kaseko, ukuaji wa sekta ya utalii utasaidia kuboresha uchumi kwa ujumla kupitia uchocheaji wa fursa za ukuaji wa biashara na uzalishaji wa ajira katika sekta mbalimbali za kiuchumi mkoani huo.

 

Zaidi Kaseko alipongeza ushirikiano baina ya viongozi wa serikali, waandaaji na waratibu, madereva, na watazamaji katika kufanikisha mashindano hayo. "Matukio kama haya yako si kama matukio ya kawaida; yamekuwa  kama makutano muhimu kwetu sote—kuunganisha benki na jamii ili kuchochea ukuaji na maendeleo ya pamoja," aliongeza, akisisitiza athari za kijamii na kiuchumi za matukio kama hayo.

 

Kaseko alifichua kwamba benki hiyo inatarajia kuwekeza katika michezo mbalimbali, ikiangazia pia michezo kama mbio za magari, golf, na masumbwi kama michezo ya ziada baada ya kuwekeza zaidi kwenye michezo ya mpira wa miguu na marathon. "Tunatambua umuhimu wa michezo katika jamii, na tumejizatiti kuendelea kuunga mkono juhudi hizi," alisisitiza.

 

Mashindano hayo ya siku mbili yalizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Kheri James, ambaye pia aliongoza sherehe ya kuyahitimisha. Katika taarifa yake, alituma pongezi za dhati kwa Benki ya NBC na wadau wote waliohusika katika kufanikisha tukio hilo, akiashiria athari ya kudumu iliyoiacha kwa jamii ya eneo hilo.

 

"Mashindano haya si tu kwamba yamevutia jamii ya Iringa bali pia yamewashawishi kwa namna kubwa," Bw. James alieleza. "Kupitia mashindano haya, tuliweza kuonyesha na kuuza bidhaa na huduma tofauti kuanzia malazi hadi vyakula vya jadi—na hivyo kufanikisha ukuaji wa utalii katika eneo hili."

 

Akizungumzia ukuaji wa baadae wa mashindano hayo, Bw James alionyesha matumaini: "Kwa kuzingatia dhamira ya NBC na ongezeko la shauku kwa mchezo huu, naamini kwa dhati kwamba mashindano ya mwaka ujao yatakuwa makubwa zaidi na yenye ushawishi zaidi kwa jamii yetu."

 

Katika mashindano hayo, timu ya Fuchs Titan Rally kutoka Tanzania ilifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza ikiwakilishwa na madereva wake wabobevu, Manveer Bird na Manmeet Bird. Tukio hilo lilikusanya umati mkubwa wa watazamaji, ikionyesha shauku ya jamii ya ndani kwa mchezo  huo na kuthibitisha nafasi ya Iringa kama kituo hai cha matukio ya namna hiyo

 

Msimamizi wa mashindano hayo, Bi. Hidaya Kamanga, naye alionyesha shukrani zake kwa jukumu muhimu la Benki ya NBC na washirika wengine. "Udhamini mzuri tuliopewa na NBC ulifanya iwezekane kuandaa tukio hili ambalo lilizidi matarajio yetu," alieleza.

 

Hata hivyo Bi Kamanga alisema madereva wengi bado wanakumbana na changamoto za kupata udhamini, hivyo kuathiri ushiriki wao katika matukio hayo ya kusisimua.

 

Akielezea shukrani zake, mshindi Bw Manveer, alipongeza jitihada za waandaaji na Benki ya NBC. "Nataka kutoa shukrani zangu za dhati kwa kila aliyeshiriki katika kuandaa tukio hili zuri. Kushiriki na madereva wengine wenye uwezo mkubwa hakika kulitupatia changamoto sana, na nilifurahia changamoto hiyo," alisisitiza Bird, akielezea ushindani aliokumbana nao kwenye mashindano hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Kheri James (wa pili kulia) akikabidhi kikombe kwa dereva Manveer Bird kutoka timu ya Fuchs Titan Rally ya Tanzania baada ya yeye na dereva mwenzake Manmeet Bird kufanikiwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye mashindano ya mbio za magari ya NBC Iringa Mkwawa Rally 2025 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Iringa Bi Josephine Temu (kulia.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Kheri James (katikati) akikabidhi tuzo maalum kwa Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC Bw Abel Kaseko (wa pili kushoto) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki ya NBC katika kufanikisha mashindano ya mbio za magari ya NBC Iringa Mkwawa Rally 2025 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa. Benki ya NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Iringa Bi Josephine Temu (kulia)

Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC Bw Abel Kaseko (kulia) akimpongeza mmoja wa madereva walioshiriki na kufanya vizuri kwenye mashindano ya mbio za magari ya NBC Iringa Mkwawa Rally 2025 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa. Benki ya NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo.


Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Iringa Bi Josephine Temu (kushoto) akimpongeza mmoja wa madereva walioshiriki na kufanya vizuri kwenye mashindano ya mbio za magari ya NBC Iringa Mkwawa Rally 2025 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa. Benki ya NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Kheri James (alieshika  bendera ya Taifa)  akipeperusha bendera ya Taifa kuashiria uzinduzi mashindano ya mbio za magari ya NBC Iringa Mkwawa Rally 2025 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa. Benki ya NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Iringa Bi Josephine Temu (kulia)




 Wafanyakazi wa benki ya NBC wakifurahia pamoja na viongozi wa serikali, waratibu na mashabiki waliojitokeza kwenye mashindano ya mbio za magari ya NBC Iringa Mkwawa Rally 2025 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa. Benki ya NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...