• Benki ya Stanbic yazindua huduma za Private Banking jijini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa upanuzi wa huduma zake nje ya Dar es Salaam, baada ya mafanikio ya matukio kama haya Mwanza na Mbeya mapema mwaka huu.

• Upanuzi huu wa Arusha unaonesha dhamira ya Benki ya Stanbic kuwasogezea wateja wake huduma za kifedha za hali ya juu, na kuwapa fursa wajasiriamali, wataalamu na familia za wafanyabiashara nje ya Dar es Salaam kunufaika na Private Banking.

• Tukio hili limeangazia kaulimbiu ya Stanbic ya “Ujasiriamali Hauishi”, likilenga kuwawezesha wateja kwa mipango ya kifedha ya muda mrefu, huduma mahususi za Private Banking, na njia za kujenga urithi wa kifamilia wa kifedha.

Benki ya Stanbic imezindua maboresho ya huduma zake za wateja maalum rasmi huduma ya Private Banking Client Value Proposition (CVP) jijini Arusha, ikionyesha dhamira yake ya kuwawezesha Watanzania wenye ukwasi mkubwa kwa kuwapatia suluhisho bora za kifedha za kiwango cha kimataifa. Uzinduzi huu unafuatia mafanikio ya matukio kama haya yaliyofanyika Mwanza na Mbeya mapema mwaka huu, na kuonyesha mkakati wa benki wa kupeleka huduma bora za kifedha nje ya Dar es Salaam.

Kupitia huduma hii, wakazi wa Arusha wananufaika kwa kuunganishwa na suluhisho za kifedha zinazowiana na mahitaji ya kipekee ya mkoa huu. Kwa kuwa Arusha ni kitovu cha biashara ya utalii, biashara ya madini, kilimo cha mazao ya biashara , na biashara za kifamilia, Private Banking inaleta thamani halisi kwa watu wanaojenga urithi wa kifamilia kupitia kazi zao za kila siku.

Arusha imechaguliwa kwa ajili ya tukio hili muhimu kutokana na umuhimu wake wa kiuchumi na kijamii. Kama kitovu cha utalii, diplomasia, kilimo, na biashara zinazokua kwa kasi, Arusha ina jamii yenye nguvu ya viongozi wa biashara, wawekezaji na wataalamu wanaotafuta huduma za kifedha za kiwango cha juu. Pia ni lango kuu la Afrika Mashariki na makao ya taasisi nyingi za kimataifa, hivyo kuifanya kuwa soko muhimu kwa huduma za Private Banking.

Tukio la Arusha limewakutanisha wateja maalum wa Benkiwa Private Banking, wajasiriamali na wadau wakuu kujadili jinsi huduma hizi zinavyoweza kusaidia kukuza, kusimamia, na kulinda utajiri wa kifamilia kwa vizazi vijavyo. Kwa kauli mbiu ya 'Ujasiriamali Hauishi,' tukio hili limeangazia umuhimu wa mipango ya kifedha ya muda mrefu, urithi wa kifedha, na huduma za kipekee zinazolenga tabaka la juu la Tanzania.

Arnold Shirima, mtoa huduma za utalii kutoka Usa River, alishiriki uzoefu wake,

“Huduma hii imenisaidia kupanga kwa mikakati zaidi kuhusu mustakabali wa biashara yangu. Kama mtu anayesimamia mapato ya msimu, nafasi nyingi za kuhudumia wateja, na gharama kubwa za uendeshaji, nimejifunza jinsi ya kutenganisha fedha za binafsi na za biashara bila kuathiri ubora wa huduma au ukuaji wa biashara.

Kupitia msaada wa Benki ya Stanbic, sasa najisikia kuwa na udhibiti zaidi wa fedha zangu na nina uwezo bora wa kukuza biashara kwa njia endelevu.Arnold Shirima, mkulima wa mazao ya biashara katika maeneo ya Usa River, anasema: “Huduma hii imenisaidia kupanga mikakati ya kifedha ya muda mrefu. Kwa sasa ninafahamu namna ya kutenganisha fedha za biashara na matumizi binafsi bila kuathiri ukuaji wa shamba langu.”

Katika sekta ya madini, Bruno Ngowa, mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha, anasema,

“Sekta ya madini ni ya kipekee—ina changamoto zake lakini pia fursa kubwa kwa maendeleo ya kifamilia na kijamii. Kwa miaka mingi nimekuwa nikijitahidi kukuza biashara yangu kutoka kwa uchimbaji mdogo hadi kuwa mtoa huduma mwenye leseni kamili katika usambazaji wa madini ya vito.

Huduma za wateja maalum kutoka Stanbic zimenisaidia kuweka misingi imara ya kifedha kwa biashara hii. Kupitia ushauri wa kitaalamu na mipango ya kifedha niliyopatiwa, sasa ninaona kwa uwazi namna ya kulinda mali zangu, kuweka utaratibu wa kurithisha biashara hii kwa watoto wangu, na kuhakikisha kuwa mchango wangu katika sekta hii unaendelea hata baada yangu. Kwa mara ya kwanza, ninaona madini haya si tu kama bidhaa ya sasa—bali kama urithi wa familia.

”Naye Bruno Ngowa, mmiliki wa hoteli ndogo ya kifamilia mkoani Arusha, anasema: “Huduma za wateja maalum kutoka Private Banking ya Stanbic zimenipa mwanga mpya juu ya mirathi na uwekezaji kwa vizazi vijavyo. Kwa mara ya kwanza, naona njia ya kuhakikisha watoto wangu wanaendeleza biashara hii ya familia.”

Shangwe Kisanji, Mkuu wa Idara ywa Wateja Maalum wa Benki ya Stanbic Tanzania, alisisitiza umuhimu wa hatua hii: “Arusha ni jiji lenye nguvu na ujasiriamali mkubwa, na ni makazi ya baadhi ya viongozi wa biasharawafanyabiashara wabunifu zaidi nchini. Upanuzi wetu hapa unahakikisha kuwa wateja wa eneo hili wanapata moja kwa moja huduma zetu za Private Banking, kuwasaidia kufikia malengo yao kwa uhakika.”

Huduma za Wateja Maalum Private Banking za Stanbic zinajumuisha huduma za usimamizi wa mahusiano ya kifedha, ushauri wa uwekezaji, mipango ya urithi wa kifamilia, uwekezaji wa nje ya nchi, na mikopo iliyoundwa mahsusi kwa mahitaji ya wateja. Mpango huu pia umeambatana na programu za elimu ya kifedha zinazolenga kuwawezesha wateja na familia zao kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kujenga mustakabali wa kifedha imara.

Kwa kupitia huduma hizi, wateja wa Arusha si tu wanapata ushauri wa kitaalamu, bali pia wanapewa msaada wa kupanga kwa ufanisi, kulinda mali, na kurithisha utajiri wao kwa kizazi kijacho kwa amani na uhakika.

Uongozi wa huduma za wateja maalum Benki ya Stanbic pia umetambuliwa kimataifa, baada ya kutangazwa kuwa Benki Bora ya wateja maalum Tanzania kwa mwaka 2024 na Euromoney, jarida maarufu la kifedha duniani. Tuzo hii ya heshima ni uthibitisho thabiti wa dhamira ya Stanbic katika kutoa huduma bora kwa wateja, suluhisho maalum za usimamizi wa utajiri, na ushauri wa kifedha wa kisasa unaokidhi mahitaji yanayobadilika ya wateja wenye ukwasi mkubwa na wale wanaoinukia barani Afrika.

Tuzo hii inaonyesha uwezo wa benki kuunganisha mbinu bora za kimataifa na uelewa wa ndani wa soko—na hivyo kuwasilisha huduma ya Private Banking ya kiwango cha dunia inayolingana kikamilifu na mazingira na matarajio ya wateja wa Kitanzania.

Uzinduzi huu unakuja wakati Benki ya Stanbic ikisherehekea miaka 30 ya uwepo na mchango nchini Tanzania.—miaka mitatu ya mfululizo ya ukuaji jumuishi, uwezeshaji wa mafanikio ya biashara, na utoaji wa suluhisho za kifedha zenye ubunifu. Ikiwa ni benki ya tatu kwa ukubwa nchini, uwekezaji wa Stanbic kwenye miji kama Arusha unaonyesha dhamira yake ya kuunga mkono maendeleo ya taifa na kuwa karibu zaidi na wateja wake.

Uzinduzi huu unathibitisha maono ya muda mrefu ya Benki ya Stanbic ya kuwa mshirika wa kifedha wa karibu zaidi na wa kuaminika nchini Tanzania—ikiwahudumia wateja si tu Dar es Salaam, bali pia katika maeneo yote yenye fursa za kiuchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...