Na Seif Mangwangi, Michuzi TV Arusha

MKURUGENZI wa ufundi wizara ya Elimu na Sayansi nchini Dkt Fredrick Selukela amekiagiza chuo cha ufundi Arusha (ATC), kufuatilia bunifu mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi wanaomaliza masomo yao katika chuo hicho na kuziboresha ili ziweze kuwa na tija kwa Taifa ikiwemo kutoa ajira kwa watanzania.

Akizungumza kwenye kilele cha wiki ya ubunifu inayofanywa na wanafunzi wa mwaka wa mwisho wanaosomea fani mbalimbali katika ngazi za Diploma na shahada chuoni hapo, Dkt Selukela amesema lengo la Wizara na chuo hicho ni kuandaa wataalam watakaofanya bunifu zenye tija kwa Taifa.

Amesema pamoja na kuwepo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi, lakini yeye anawapongeza wote kwa kazi waliyofanya kwa kuwa wametumia muda wao mwingi kufikiri na kutengeneza bunifu zao.

" Mkuu wa chuo naomba ufuatilie hizi bunifu na kuhakikisha zinaboreshwa zaidi, wanafunzi mshikeni mkuu wa chuo, muhakikishe kile mlichogundua mnakiboresha zaidi na kifanye kazi, kwa kufanya hivi mambo mengi yatarahisishwa,"amesema.

Mkuu wa chuo hicho Profesa Musa Chacha amesema bunifu ambazo zimekuwa zikifanywa na wanafunzi chuoni hapo zimewezesha wengi wao kujiajiri na kuondokana na tatizo la ajira.

Amesema chuo kitaendelea kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kufanya tafiti na kufanya bunifu mbalimbali zitazorahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika jamii.

Katika maonyesho hayo, wanafunzi waliweza kuonyesha bunifu mbalimnalj katika sekta ya kilimo, utalii, teknolojia za afya, umeme, maji na teknolojia ya Habari na mawasiliano.

Moja ya bunifu iliyofanywa ni pamoja na mashine ya kukuza mishipa ya damu ili kumrahishishia daktari kuchoma sindano kwa urahisi iliyofanywa na wanafunzi wa Diploma, Hanan Mohamed, akishirikiana na wenzake Petronila Fella na Farsiya Juma.

Bunifu nyingine ni pamoja na mashine ya kufuatilia matumizi ya gesi, teknolojia ya matumizi ya QR Code, utengenezaji wa ndege nyuki (drone).
Mkurugenzi wa Ufundi Wiizara ya Elimu na Sayansi Dkt Fredrick Selukela
Mkuu wa Chuo cha ufundi Arusha (ATC), Profesa Musa Chacha




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...