Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Kaspar Mmuya amewataka Watendaji wa Mitaa na Vijiji kuhakikisha wananchi wanapewa nafasi ya kupendekeza majina ya Barabara na Mitaa yao pamoja na kutatua changamoto zote za majina ya Barabara hizo.
Katibu Tawala huyo amesema hayo leo Jijini Dodoma Mei 26,2025 katika hafla ya ufunguzi wa uhakiki wa taarifa za Anwani za Makazi Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa.
"Mkawasaidie wananchi kuhakikisha changamoto zote za majina ya Barabara zinatatuliwa kikamilifu pamoja na kuhakikisha wanapewa nafasi ya kupendekeza majina ya Barabara na mitaa yao".
Na kuwataka Watendaji hao kuhakikisha taarifa za Anwani za Makazi zinahakikiwa kikamilifu kwani Hategemei kuona Mtendaji yeyote ana taarifa zenye mapungufu na zisizo sahihi katika mtaa au Kijiji chake kwani taarifa hizo ni muhimu kwa ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla.
Pia amewaomba Wananchi wa Jiji la Dodoma na Mkoa mzima kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kuhakiki taarifa za Anwani zao, na ni matarajio kuwa baada ya zoezi hili, kila mmoja ataweza kufahamu Anwani yake ya Makazi na kujenga utamaduni wa kujitambulisha kwa kutumia Anwani hizo.
Kwa upande wake Josephine Mwaijande ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimaliwatu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameseam mpaka sasa zoezi la kuhakiki taarifa limekamilika kwenye Halmashauri zaidi ya 40 ambapo katika Halmashauri hizo wameweza kusajili na kutoa anwani mpya 535,856 ikiwa ni ongezeko la makazi mapya.
"Utekelezaji wa Mfumo wa NaPA ni zoezi endelevu kwa kuwa Teknolojia zinabadilika na mahitaji ya watumiaji yanaongezeka. Kwa kutambua hilo, Wizara inaratibu zoezi la kuhuisha taarifa ili kuendelea kuwa na taarifa sahihi zenye tija kwa Taifa letu".
"Hadi sasa zoezi la kuhakiki taarifa limekamilika kwenye Halmashauri zaidi ya 40 wakati juhudi zikiendelea ili kukamilisha zoezi hili katika Halmashauri nyingine. Katika Halmashauri zilizohakikiwa tumeweza kusajili na kutoa Anwani mpya 535,856 hii inathibitisha ongezeko la makazi mapya ambayo yanahitaji kupatiwa Anwani".
Na kuongeza kuwa Wizara imejipanga kuendelea kujenga uwezo kwa wataalam na watendaji katika ngazi zote ili kujenga uendelevu wa utekelezaji wa shughuli zote za Mfumo ambapo hadi sasa zaidi ya wataalam na watendaji 9,072 wamejengewa uwezo, na hata hivyo, katika kutekeleza zoezi lililo mbele yao timu ya wataalam za Wizara itashirikiana na wataalam wa Mkoa na Halmashauri zote katika kufanikisha zoezi hilo na matarajio ni kuwa zoezi litatekelezwa kwa ufanisi unaohitajika.
Naye Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe amesema Halmashauri ya Jiji la Dodoma ndio wanufaika wakubwa wa zoezi hili kutokana na kasi ya ukuaji wa Jiji la Dodoma,ongezeko la idadi ya makazi na idadi ya wakazi wanaohamia katika Jiji hili.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...