NA EMMANUEL MBATILO,
TAASISI ya HakiElimu imeishauri Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha angalau asilimia 15 ya bajeti ya taifa ya 2025/26 inatengwa kwajili ya sekta ya elimu ambapo wanatarajia ongezeko la shilingi trilioni 2.08 katika bajeti ya sekta ya elimu kutoka shilingi trilioni 6.17 ya mwaka 2024/25 hadi kufikia shilingi trilioni 8.25 mwaka wa fedha 2025/26.
Kwa kuwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali Mwaka 2025/26, bajeti ya serikali inakadiriwa kufikia shilingi trilioni 55.06, sawa na ongezeko la asilimia 11.5 kutoka bajeti ya mwaka 2024/25.
Ameyasema hayo leo Mei 5, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage wakati wakitoa Mapendekezo katika Mpango na Bajeti ya Sekta ya Elimu Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Dkt. Kalage amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali ilitenga na kuidhinisha kiasi cha shilingi trilioni 6.17 kwaajili ya Sekta ya Elimu, sawa na asilimia 12.5 ya bajeti ya taifa iliyokuwa shilingi trilioni 49.35.
"Kiasi hiki sio tu kilikuwa chini ya kiwango kilichopendekezwa na Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Elimu (ESDP III) cha shilingi trilioni 6.64, bali pia ni chini ya makubaliano ya kikanda, hususan azimio la Incheon (Incheon Declaration, 2015) linaloagiza mataifa kutenga angalau asilimia 4 – 6% ya Pato la Taifa (GDP) na/au 15% hadi 20% ya bajeti ya taifa katika ya elimu. Tanzania imekuwa na mwenendo usioridhisha katika kufikia azma hii kwa kushindwa kufikia walau 15% ya bajeti ya taifa kwa miaka mitano mfululizo". Amesema Dkt. Kalage.
Aidha Dkt. Kalage amesema kutokana na uwepo wa uhaba wa walimu nchini, wanaishauri Serikali kuja na mkakati wa muda mfupi wenye hatua mahususi za kuongeza idadi ya walimu kwa haraka ambao unapaswa kuambatana na mpango wa bajeti madhubuti ili kuhakikisha utekelezaji wake.
"Katika upangaji wa bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2025/2026, tunapendekeza Serikali itenge bajeti maalum kwa ajili ya kuajiri walimu wapya wasiopungua 40,000 kila mwaka ili kupunguza uhaba wa walimu kwa kipindi cha miaka 5". Amesema
Amesema kuwa ripoti ya Wizara ya TAMISEMI mwaka 2024 kwa Kamati ya Bunge ya Elimu imeonyesha kuwa shule za awali zina upungufu wa walimu 61,559, shule za msingi 124,826, na shule za sekondari 82,517. Hii inafanya jumla ya upungufu wa walimu katika shule za msingi na sekondari kufikia walimu 268,902.
Amesema masomo ya sayansi yana upungufu mkubwa wa walimu ikiongozwa na somo la Sayansi ya Uhandisi lenye upungufu wa asilimia 81.43%, Elektroniki na Kompyuta asilimia 73%, Baiolojia 58%, Kemia 52%, na Fizikia asilimia 53.35%.
Pamoja na hayo amesema katika utafiti wao walioufanya kwenye shule kadha za umma na binafsi umebaini changamoto kubwa ya uwepo wa vitabu husika licha ya taarifa ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuonesha kuwa hali ya upatikanaji wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia katika ngazi ya elimu ya awali, msingi, sekondari na elimu ya ualimu nchini imeendelea kuimarika.
Amesema taarifa ya HakiElimu inasadifu ripoti kuu ya mwaka ya Ukaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2022/23 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mwezi Machi 2024, inayoonesha kutosambazwa kwa vitabu vya kiada vyenye thamani ya Sh. bilioni 10.6 ambavyo OR-TAMISEMI ililipa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya shule za msingi Tanzania Bara ambapo kunazorotesha utoaji wa elimu bora na huenda ikawa ngumu kufikia lengo la uwiano 1:1 wa kitabu kwa mwanafunzi ifikapo 2025/26.
"Rai yetu kwa Serikali kutenga na kuidhinisha bajeti kwa ajili ya kuandika na kuchapa vitabu vya kiada na viongozi vya walimu Elimu ya Msingi kwa lugha ya Kingereza na Elimu ya Sekondari kidato cha 1-5, Stadi za Maisha, vitabu hivi ambavyo havikuandikwa katika kipindi cha nusu mwaka 2024/25, sambamba na uandishi wa maudhui ya kielekroniki ili kukabiliana na mahitaji yanayotokana na ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa elimu ya awali, msingi na sekondari kila mwaka". Ameeleza Dkt. Kalage.

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa Mapendekezo ya HakiElimu katika Mpango na Bajeti ya Sekta ya Elimu Mwaka wa Fedha 2025/2026 leo Mei 5, 2025 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa Mapendekezo ya HakiElimu katika Mpango na Bajeti ya Sekta ya Elimu Mwaka wa Fedha 2025/2026 leo Mei 5, 2025 Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uvumbuzi na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, Mwemezi Makumba akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa Mapendekezo ya HakiElimu katika Mpango na Bajeti ya Sekta ya Elimu Mwaka wa Fedha 2025/2026 leo Mei 5, 2025 Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uvumbuzi na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, Mwemezi Makumba akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa Mapendekezo ya HakiElimu katika Mpango na Bajeti ya Sekta ya Elimu Mwaka wa Fedha 2025/2026 leo Mei 5, 2025 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...