Na Oscar Assenga, Tanga
Tanga Yetu kupitia mradi wa Fursa kwa Vijana (GOYN TANGA ) kwa
kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania wametoa mafunzo kwa ajili ya
utengenezaji wa filamu kwa wasanii mkoani Tanga ili waweze kuwa waandaaji
wazuri ambao watafanya vizuri kupitia tasnia hiyo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Filamu
kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Ally Makata kwa niaba ya Serikali alisema kwamba
wamekuja Tanga mara ya pili kutoa mafunzo kuhusu utengenezaji wa filamu kwa
wasanii wa filamu mkoani Tanga.
Alisema kwamba mafunzo hayo waliyatoa kwa awamu tatu ambapo ya kwanza ilikuwa ni watu wakwenda kufanya utafiti watu wapate wazo kwamba endapo watapata muongozo nani anaweza kucheza na bajeti ya kiasi gani na nani anaweza kufadhili ikiwemo kutengeneza hadithi fupi fupi lazima mdau yoyote kwenye filamu aweza kufanya hivyo ili aweze kufanya vizuri.
Aidha alisema kwamba baada ya hapo awamu ya pili na tatu ni
kushika Kamera kuona namna kutengeneza mwanga na watu kwenda kwenye maeneo
husika na uhariri pamoja na namna ya kupanga na kutengeneza sauti ili uweza
kupata picha kamili na viti vyengine.
“Tunawashukuru Tanga Yetu kwa kuweza kufadhili na kushirikiana
na Bodi ya Filamu nchini kwa watayarishaji wa Mkoa wa Tanga waweze kupata
maarifa kutokana na kwamba Tanga kwa asilimia kubwa ipo chini na watayarishaji wa Tanga
wanalalamika kwenye media wanaoka kazi za mikoa mengine na ikitokea tuzo mikoa
mwengine inashika tuzo”Alisema
“Wakati ukiangalia Tanga kuna rasimali za kila kitu ukiangalia
mandhara wana sehemu za vivutio wana mazingira mazuri tamaduni wana vyakula
tamaduni watu wanaishi kila siku kwanini tusipate Filamu inayoakisi Jamii ya
Mkoa wa Tanga “Alisema
Alisema kwamba ukiangalia Marehemu King Majuto ameshaandoka
ambaye alikuwa anaiwakilisha vizuri mkoa wa Tanga ikiwemo Marehemu Bauji
tunapata stori kulikuwa na waandishi wazuri na waigizaji wazuri lakini sasa
haifanyiki hivyo shabaha kubwa ya Dkt Omari na Taasisi ya Tanga Yetu ni kuona namna
Tanga inarudi upya.
Alisema wanawapatia mafunzo na maarifa ili kesho na kesho kutwa
waweze kufanya vizuri mkoa wa Tanga ili waweze kufanya vziuri na kurejesha
katika hali yake ya kawaida na kung’ara vziuri.
Alisema waliamua kushirikiana na Bodi ya Filamu kama Taasisi ya Serikali waliamini kama wana majukumu ya kusimamia,kuhamasisha na kutangaza hiyo sekta kwa hiyo walikubaliana kuendelea na kusaidia hayo mafunzo yaliyoanza kwenye uzalishaji na wazo kubwa ni kuhakikisha vijana wanapata uzoefu kwenye sekta binafasi ambazo zinashirikiana na bodi ya filamu.
“Leo imefikia mwisho wa awamu ya pili na tutaenda kwenye awamu
ya tatu kuzalisha filamu ambazo zitakwenda kwenye soko hivyo niwaombe wadau
mbalimbali hao vijana wapo vizuri ni kuwaamini na kuwapa kazi ambazo wanaweza
kufanya nao wataweza kuwasaidia”Alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...