Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, ameihakikishia Finland kuwa Zanzibar iko tayari kushirikiana nayo katika kuhakikisha malengo ya kuwakomboa wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya udhalilishaji, ukatili wa kijinsia na umasikini yanafikiwa.
Mama Mariam ameyasema hayo alipokutana na Mke wa Rais wa Finland, Bi Suzanne Innes Stubb, aliyezuru Ofisi za ZMBF zilizopo Migombani, tarehe 15 Mei 2025.
Aidha, Mama Mariam Mwinyi amesema kuwa ZMBF imekuwa ikiendeleza ushirikiano na taasisi mbalimbali, wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa, ili kufanikisha dhamira na malengo ya taasisi hiyo. Ametoa wito kwa Finland kushirikiana na ZMBF kwa ukaribu zaidi ili kuimarisha juhudi hizo.
Ameeleza kuwa lengo kuu la taasisi hiyo ni kuwawezesha wanawake kijamii na kiuchumi, pamoja na kuhakikisha ustawi wa watoto na wanafunzi wa kike kwa kuwaelimisha juu ya haki zao na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.
Mama Mariam ameeleza kuwa mikakati ya ZMBF inajumuisha utoaji wa elimu ya lishe na uzazi salama kwa akina mama, hatua iliyosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Pia ameelezea jitihada za ugawaji wa taulo za kike (Tumaini Kits) kwa wanafunzi wa kike, hatua inayowawezesha kusoma katika mazingira salama na yenye staha.
Kuhusu sekta ya kilimo, Mama Mariam amebainisha kuwa ZMBF imeendelea kuwajengea uwezo wakulima wa mwani, hususan wanawake kwa kuongeza thamani ya bidhaa wanazozalisha na kuboresha ubora wa mwani ili kupata bei nzuri katika masoko.
Vile vile, ameeleza kuwa ZMBF imeweka mkakati maalum wa kutumia majukwaa mbalimbali kulinda watoto dhidi ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.
Mama Mariam ameiomba Finland kuendeleza ushirikiano huo na kuunga mkono juhudi hizo kupitia misaada na programu mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili.
Kwa upande wake, Mke wa Rais wa Finland, Bi Suzanne Innes Stubb, amesema kuwa amefurahishwa na ushirikiano uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 kati ya Tanzania na Finland, na ameahidi kuendeleza uhusiano huo katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Ameipongeza ZMBF kwa malengo na mafanikio yake katika kuimarisha ustawi wa jamii, kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, kuendeleza usawa wa kijamii, na kuboresha afya ya mama na mtoto, pamoja na hatua zilizopigwa na Zanzibar katika kuendeleza kilimo cha mwani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...