Na.Vero Ignatus Arusha.
Kukosekana kwa sera ya nyumba ya Taifa kumeelezwa kuwa ni mojawapo ya sababu ya kukosekana kwa thamani halisi ya yamiliki ya makazi na biashara,na kuchangia ujenzi holela na makazi duni katika maeneo mbalimbali nchini
Hayo yameibuka baada ya mada kuhusu uhusiano wa nyumba na miliki iliyowasilishwa na mtaalam wa Ardhi na nyumba ,mstaafu chuo cha ardhi Prof.Joseph Lussuga Kironde katika mkutano mkuu wa tano wa Miliki Tanzania unaofanyika leo mei 15,2025 Jijini Arusha katika Hotel ya Mountmeru na kusema kuwa shirika la kwanza kuanzishwa lilikuwa shirika la nyumba la Taifa ambapo ulififia miaka ya 1990 na serikali kuhamia zaidi kwenye masuala ya viwanja,ambapo viwanja vikawa havitoshi watu wakawa wanajijenge kiholela .
‘’Kwa mawazo yangu hili la watu kujijengea huenda limeondoa ule msukumo wa kwa watu,lakini ukiangalia nyumba walizojenga nyingi hazijaisha zinakuwa kama nyumba zetu ni working progress unajengawee hadi utakapochoka na zipo katika maeneo ambayo hayajapimwa,Ndiyo maana tunasema kwamba nchi inahitaji SERA YA NYUMBA,Kwani sera zinakuja na sharia zake na mipangilio yake na sera hii ikiwemo itatusaidia sana,napendekeza kwamba suala la nyumba liwe kwenye Vision ya Taifa .Alisema Prof. Kironde.
Akizungumza katika Komgamano hilo la tano Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Deogratius Ndejembi amesema kuwa Serikali inaendelea na mkakati wa kuboresha sera ya nyumba na makazi ,ili kuendana na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi ikiwemo ongezeko la watu na mahitaji ya makazi bora lengo likiwa ni kuwa na sera moja jumuishi itakayowezesha uundaji, usimamizi na uendelezaji wa sekta hiyo.
Aidha ametoa rai kwa wataalam wote wa nchini na Kanda ya Afrika ya Mashariki kuhakikisha wanadumisha maadili kazi kuheshimu miiko,taaluma zao kuendeleza ushirikiano wa taaluma ndani na nje ya nchi,kwani ushirikiano huo ndio utakaoifanya Afrika Mashariki kuwa kitovu cha maendeleo,amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuratibu na kusimamia kuendeleza sekta hiyo nchini ili kuhakikisha haki za wadau zinalindwa na taaluma hiyo inakuwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo.
Vilevile Mhe.Ndejembi amewakaribisha sekta binafsi kuweza kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kwamba kushirikiana kwa pamoja kutapelekea wananchi kuwa na makazi bora ya kisasa,kwani serikali ya awamu ya sita inafanya mambo mengi katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nyumba za bei nafuu kwa watanzania walio wengi.
‘’Mnapoona kuna suala ambalo tunaweza kushirikiana na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vilevile Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar sisi tupo tayari kushiriki pamoja nanyi ,maana tunataka kuona ile dhamira ya watangulizi wetu tangu tupate uhuru wetu.Alisema
Kwa kupande wake rais wa chama cha wataalam wa Miliki Tanzania (AREPTA) Andrew Peter Kato amesema huo ni mkutano wao wa Mwaka a mbapo wamekutana wataalam tofauti wakiwemo Maafisa Ardhi ,Wathamini,Wataalam wanaofanya uchambuzi yakinifu wa miradi yay a Miliki,kwa paoja watajadili na kufanya uwasilishaji wa kuhusiana na matokeo chanya ya yanayotokana na uboreshaji wa miundombinu Afrika ya Mashariki
Kato amesema vilevile wameshirikiana na Jumuiya ya Wataalam wa miliki Afrika ,kwa upande wa Afrika ya mashariki(AfRES) .ambapo wanaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘’Uboreshaji wa miundombinu,ya usafiri katika miliki/katika kuongeza thamani ya ardhi Afrika ya Mashariki’’ ,ambapo wanaangazia zaidi katika uboreshaji wa miundombinu haswa mabasi yaendayokasi na Reli katika kuongeza thamani ya ardhi.
"Nafasi yetu ukienda kwa wananchi kwa wananchi kwenye halmashauri tunaongelea maafisa ardhi kumekuwa na mkanganyiko kwa maana ya kamishna wa ardhi chini yake ana vitengo tofauti kuna mkurugrnzi wa mipango miji au afisa mipangomiji kwa ngazi ya halmashauri kuna mpima ardhi kuna mmilikishaji na mthamini kwahiyo utaona kuna idara tofauti wengi wanawaita afsa ardhi kwa wananchi wa kawaida".Alisema
Amesema kwa ngazi ya Halmashauri wanachama wao ni wathamini wanaothamini mali wanaponunua nyumba au kufanya uaulishaji kutoka miliki moja kwenda nyingine ili ifanyiwe uthaminishaji ,au kulipa kodi ya ardhi lazima mthamini athaminishe,vilevile kuweka bima lazima mthamini athaminishe mali au mtu anapohitaji kuchukua mkopo.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan alisema kuwa SERA ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 Toleo la Mwaka 2023 iliyozinduliwa machi 17,2025 Jijini Dodoma ina lengo la kuhakikisha nchi inakuwa na mfumo wa umiliki ,upatikanaji na usimamizi wa matumizi ya ardhi kwa maendeleo endelevu na haijabadilika.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...