Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira akiwa na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mbeya Vijijini, Ndg.Gidion G.Mapunda ofisi kwake baada ya kufika kwa ajili ya kuona zoezi la Uboreshaji linavyokwenda katika Jimbo hilo.

Sambamba na hilo Mhe.Rwebangira ametembelea na kukagua vituo vya kuandikisha Wapiga Kura vya Shule ya Msingi Nsalala na Ofisi ya Mtendaji Kata ya Nsalala vyote vilivyopo katika kata ya Nsalala na Kituo cha Mwenyekiti wa Stendi Tarafani kilichopo katika Kata ya Utengule Usongwe.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya Pili, mzunguko wa kwanza na uwekaji wazi wa Daftari la awali kwa mikoa 15 nchini ikiwemo na mkoa wa Rukwa ambapo umeanza tarehe 01 Mei, 2025 hadi tarehe 07 Mei, 2025 ambapo vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...