Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa muda wa wiki mbili kwa uongozi wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga eneo la kariakoo kuanza kufungua njia ili kuruhushu shughuli za kibiashara kufanyika kwa ufanisi wakati serikali ikielekea kufanya uzinduzi wa soko jipya la Kariakoo

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari  RC Chalamila amesema wanapoelekea kwenye uzinduzi wa soko jipya ni muhimu kwa Machinga kariakoo kufungua njia za kuingia ili kupeleka bidhaa kwenye soko jipya la kariakoo kwani soko hilo limeshakamilika kwa asilimia 98 hivyo ni muhimu njia zikawa wazi na ametoa muda wa wiki mbili kuanzia leo Mei 28,2025.

RC Chalamila amesema kuwa wafanyabiashara wadogo watakaoondoshwa kwenye njia hizo zinazopaswa kufunguliwa watapelekwa kwenye maeneo maalum yanayotengwa kwani Serikali inatambua uwepo wa machinga kwenye eneo hilo kama ambavyo wizara ya TAMISEMI imeshaelekeza

Aidha RC Chalamila amezungumzia suala la wafanyabiashara waliokuwepo kwenye Soko la Kariakoo hapo awali kabla halijaungua ambapo amesema wote waliokuwepo kuhakikiwa na watajejeshwa kama ambavyo Rais Dkt Samia alivyoelekeza na watapaswa kufuata taratibu ikiwemo kujaza mikataba na kujiandaa kulipa kodi na kwamba Mkoa huo umefanikiwa kuondoa udalali wa upangishaji maeneo na sasa mfumo wa kidijitali ndio unatumika.

Kwa upande wake Meneja Mkuu shirika la Masoko Kariakoo Ashrafu Abdulkarim amesema Shirika hilo linaendelea kuratibu wafanyabiashara waliokuwepo kurejea kwenye Soko hilo ambapo kwa idadi walikuwa 1520 lakini hadi sasa waliojisajili kwenye mfumo na kujaza fomu ni wafanyabiashara 1159 na kusema kuwa maeneo mengine ya wazi yaliyobaki yatatangazwa kupitia mfumo wa TAUSI ili yapate wapangaji






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...