RIZIKI Shahari Mngwali Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Mafia.
Riziki, akichukua fomu hiyo amesema kuwa matamanio yake ni kupambania maslahi ya watu wa kisiwa hicho pamoja na usafiri bora wa kuingia na kutoka pamoja na miondombinu ya ndani ya kisiwa hicho.
Amesisitiza kupigania Ustawi wa wavuvi, Elimu bora , afya , pamoja na migogoro ya ardhi inayotokana na uwekezaji usiojali wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...