Na Janeth Raphael MichuziTv- Bungeni -Dodoma

WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inajivunia kuunganisha mifumo ya takwimu za elimu na kuwa na mfumo mmoja wa sekta ya elimu.

Hayo yameelezwa leo Mei 12,2025 bungeni na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Waziri Mkenda amesema takwimu za elimu ni nyenzo muhimu katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji, kufanya tafiti na kutoa maamuzi mbalimbali.

"Kwa kutambua umuhimu huo, Serikali imeunganisha mifumo ya takwimu za elimu na kuwa na mfumo mmoja wa sekta ya elimu,"amesema Waziri Mkenda

Aidha,Wizara imeendelea na ujenzi wa Mfumo wa Takwimu wa Sekta ya Elimu utakaowezesha upatikanaji wa takwimu zote za sekta kupitia mfumo huo.

Aidha, mfumo huo utakuwa na uwezo wa kupokea takwimu mbalimbali zinazohusiana na elimu kutoka katika mifumo mingine ya Serikali ikiwemo NIDA, RITA, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Idara ya Uhamiaji na OR–TAMISEMI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...