Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amewahimiza Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura kwa awamu ya pili ambapo zoezi hilo linalotarajiwa kuanza mnamo tarehe 16 hadi 22 Mei 2025 katika ofisi zote za Kata Mkoani Dodoma.

Mhe Senyamule amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari akitoa Taarifa juu ya uboreshaji wa Daftari hilo la mpiga kura kwa awamu ya pili Mkoani Dodoma.

Na kusema kuwa ni muhimu kwa wapiga kura kuhakikisha kuwa taarifa zilizopo kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ni sahihi ili waweze kutimiza haki yao ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

"Zoezi hili ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu,hivyo naomba niendelee kusisitiza kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura tarehe 16 hasi 22 Mei alike kituoni kwaajili ya kuhakiki Taarifa zake".

Aidha amesema uboreshaji wa Daftari wa awamu hii ya pili utahusisha kuandikisha wapiga kura wapya wenye miaka 18 na kuendelea ambao hawakujiandikisha na ambao watatimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Pia wapiga kura kuhakiki taarifa zao,kufanya marekebisho ya taarifa na kuweka pingamizi kwa wapiga kura wasio na sifa ya kuendelea kuwemo kwenye daftrai.

Uboreshaji huu utafanyika katika Mkoa wote wa Dodoma ambapo idadi ya Vituo kwa Mkoa mzima ni 413,huku idadi kwa kila Halmashauri ikiwa ni Halmashauri ya Chemba vituo 58,Jiji la Dodoma vituo 105,Kongwa vituo 41,Mpwapwa vituo 67,Bahi vituo 32,Kondoa Vijijini vituo 44,Kondoa Mji vituo 16 na Chamwino vituo 50.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...