Mbunge wa Jimbo la Solwa Mkoani Shinyanga Mhe. Ahmed Ally Salum akionesha Fomu baada ya kuchukua Fomu ya Maombi ya Kugombea Nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Solwa kupitia Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) leo Juni 28,2025.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mbunge wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga, Mhe. Ahmed Ally Salum, leo Juni 28, 2025, ameonesha nia ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kugombea tena nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.


Mhe. Ahmed Salum, ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa tangu mwaka 2005, ambapo mara baada ya kuchukua fomu, ameonekana mwenye furaha na matumaini makubwa ya kuendelea na dhamana hiyo ya kuwatumikia wananchi.


"Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutufikisha mpaka siku ya leo tukiwa wazima, lakini pia nakishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kuniamini. Leo nimechukua fomu kwa nia ya kugombea kwa awamu nyingine tena Ubunge katika Jimbo la Solwa, kuteuliwa kugombea ni kitu kingine,chama kitafanya maamuzi ya nani anafaa kuwa mbunge wa Jimbo la Solwa",amesema Ahmed Salum.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...