
ALIYEWAHI kuwa Katibu wa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ameingia rasmi katika kinyang’anyiro cha ubunge kwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Sengerema kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Hatua ya Bw. Samike kuchukua fomu imezua msisimko mkubwa katika jimbo hilo, huku wakazi na wachambuzi wa siasa wakitaja jina lake kuwa miongoni mwa wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda.
Kwa rekodi yake ya kuwa karibu na utendaji wa Hayati Rais Magufuli, pamoja na uzoefu alioupata akiwa Ikulu, wengi wanaamini kuwa ana uwezo wa kulitumikia jimbo hilo kwa weledi na kwa kasi inayotarajiwa.
Utafiti wa awali unaonesha ongezeko la uungwaji mkono kwa Bw. Samike, hasa kutokana na mvuto wake kisiasa na maono aliyoanza kuyawasilisha kwa wananchi wa Sengerema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...