Kada wa Chama cha Mapinduzi, CPA (T) Ruth Hassani akisaini kitabu.

Akiwa ameambatana na Mumewe Bw. Banyinga Majeshi, CPA Ruth ambaye ni Mhasibu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Moprogoro alichukua fomu hiyo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Same na kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya, Ndg.Amos Kusakula leo Juni 29,2025.
Ruth amesema nia yake si kutafuta nafasi ya uongozi katika jimbo la Same Mashariki bali kuwasemea Wanasame Mashariki na kusaidiana nao kutatua kero mbalimbali zinazowakabili katika jimbo hilo na Same kwa ujumla akiangazia masuala ya elimu, huduma za Afya, Maji na nisshati safi.
Katika kuwania uteuzi ndani ya Chama pia Mbunge anayemaliza muda wake Bi. Anne Kilango Malecela na Kada mwingine Bi. Miriam Mjema ni mingoni mwa wana CCM waliochukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea Ubge katika jimbo la Same Mashariki.
Jimbo la Same Mashariki lilianzishwa mnamo mwaka 1995 ambapo lilizaliwa kutoka Jimbo la Same hivyo ni moja ya majimbo mawili yanayoiunda Wilaya ya Same na ni moja ya majimbo tisa yanayounda mkoa wa Kilimanjaro.
Jimbo hilo linaundwa na Kata 14 ambapo Kata 5 ziko ukanda wa Tambarare na Kata 9 ziko ukanda wa milimani aidha lina vijiji 49 vyenye kaya 131350.
Wananchi wa Jimbo hilo kwa kiasi kikubwa wanajishughulisha na shughuli za kilimo cha Mpunga, Tangawizi, Mahindi, Maharagwe, Karanga, Ndizi, Kahawa, matunda na miti kwa ajili ya mbao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...