Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Kamishna wa wa Polisi CP Suzan Kaganda amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare, Zimbabwe leo Juni 05,2025.

Wakati wa wasilisho hilo, Mhe. Balozi Kaganda alipata wasaa wa kufanya mazungumzo na  Mheshimiwa Rais Mnangagwa na kuwasilisha  salaam za  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe hususan katika utekelezaji wa Sera ya  Diplomasia ya Uchumi pamoja na ukamilishaji wa mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili kwenye sekta za afya, elimu,kilimo na madini.

Mhe. Rais Mnangagwa alimhakikishia Mhe. Balozi Kaganda Ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na kuongeza kuwa, Zimbabwe inatambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na Tanzania katika kuhakikisha kuwa, Taifa hilo na mataifa mengine Kusini mwa Afrika yanapata uhuru wake.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...