Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) ameipongeza familia ya Chifu wa Kabila la Wahehe Adam Abdul Sapi Mkwawa II kwa kuendelea kushirikiana vyema na Serikali katika uhifadhi endelevu wa historia adhimu ya Chifu Mkwawa.

Mhe. Chana ameyasema hayo leo Juni 5, 2025 Jijini Dodoma alipofunga kikao baina ya wataalam wa Wizara hiyo na Familia ya Chifu Mkwawa kilicholenga kujadili uhifadhi endelevu wa eneo la Kalenga ambalo ni ngome ya aliekuwa Chifu wa kabila la Wahehe, Mkoani Iringa.

Aidha, Mhe. Chana ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Mikoa na Wilaya nchini kuvitambua vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo yao na kisha kupendekeza kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuvitangaza kuwa vivutio vya utalii.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia Maliasili ), CP Benedict Wakulyamba, Mkurugenzi wa Idara ya Malikale, Dkt. Christowaja Ntandu na baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Wizarani na TANAPA.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...