kutoka kushoto:Asupya Nalingigwa (Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Rejareja), Lameck Mushi (Afisa Mkuu wa Huduma za Kidijitali), na Nandi Mwiyombella (Mkuu wa Masoko na Mawasiliano) wakati wa uzinduzi rasmi uliofanyika katika Makao Makuu ya Benki jijini Dar es Salaam.


KATIKA hatua ya kuendeleza matumizi ya huduma za benki za kidijitali na kuimarisha ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania, BANK OF AFRICA – TANZANIA imetangaza uzinduzi rasmi wa “MIAMALA NI FURSA,” kampeni ya miezi mitatu ya huduma ya benki kwa njia ya simu inayowawezesha wateja kujishindia fedha taslimu kila wiki.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Huduma za Kidijitali Lameck Mushi ameeleza kuwa benki imekuja na kampeni ambayo inahamasisha na kuwapa wateja kitu cha ziada wanapofanya miamala yao ya kila siku kupitia simu za zao za mkononi.

Katika kampeni hii ya Miamala ni Fursa, wateja sasa wanaweza kushinda zawadi kwa kufanya miamala ya kibenki kupitia simu zao.

"Kampeni hii ya Miamala ni Fursa itaendeshwa kwa kipindi cha miezi 3 kuanzia June 4 hadi Septemba 3  2025 ambapo  lila wiki, wateja  watano watajishindia shilingi 50,000 kila mmoja na mwishoni mwa kampeni mshindi wa jumla ataondoka na kitita cha shilingi Milioni tano.

Mushi amesema ili kuingia katika droo ya kila wiki, mteja anatakiwa kufanya miamala mitatu au zaidi ya kuhamisha pesa kutoka benki kwenda mitandao ya simu Pamoja na muamala angalu mmoja wa aina tofauti mfano kulipa bili,kununua LUKU, kununua muda wa maongezi kwa wiki kupitia simu (B-Mobile).

Mwishoni mwa kampeni, wateja watakaokamilisha angalau miamala 36 ya kuhamisha  pesa kutoka benki kwenda kwenye mitandao ya simu pamoja na miamala 12 ya aina tofauti kupitia B-Mobile, wataingia kwenye droo ya mwisho na mshindi atakayeibuka wa kwanza ataondoka na kitita cha shilingi milioni tano.

Amesema ili kushiriki katika kampeni hii mteja anapaswa kujiunga na huduma  ya benki kwa njia ya simu ya Bank of Africa (B-mobile) au kujisajili mwenyewe bila kufika tawini kwa haraka na urahisi. Ingia PlayStore au AppStore na upakue aplikesheni yetu inayoitwa ‘’B-Mobile Bank Of Africa Tanzania’’ kisha bonyeza ‘’Get started’’ na ufuate maelekezo.,

Fanya miamala angalau mitatu ya kutuma pesa kutoka benki Kwenda mitandao ya simu Pamoja na muamala angalau mmoja wa tofauti mfano kulipa bili, kununua LUKU, malipo ya serikali kila wiki

Kampeni hii inazingatia na kufuata kanuni na sheria zote zinazotolewa na mamlaka husika ikiwemo bodi ya bahati nasibu Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi (Retail Banking), Asupya Nalingigwa, ameongeza: "Tunaleta huduma za benki karibu na hali halisi ya kila siku ya watanzania. Iwe unalipa bili, unatuma pesa kwa mwanafamilia, au unanunua muda wa maongezi - miamala yako sasa inaweza kuweka pesa kiganjani i mwako. Tuko hapa kukutuza uaminifu na kila wakati."

"Tunaelewa kuwa si kila mtu anafahamu huduma za benki kwa njia ya simu, na ndiyo sababu wafanyakazi wetu-katika kila tawi kote nchini-wamejitayarisha kikamilifu kuwasajili na kuwaelimisha wateja. na uingiajiTimu yetu ya kiufundi iko tayari kuhakikisha utoaji wa huduma ni wa uhakika," alisema.

"Iwapo unahitaji usaidizi wa kujisajili, kujifunza jinsi ya kutumia huduma hii, au kuelewa manufaa yake, tuko hapa kwa ajili yako....tutahakikisha kuwa kampeni hii ni ya pamoja na inapatikana popote ulipo,. Simu yako ya mkononi sasa inaweza kuwa tawi lako-na kila muamala ni fursa kwako"

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Nandi Mwiyombella, amesema kampeni hiyo pia ni hatua ya kujumuisha zaidi: "Hii si tu kuhusu zawadi-ni kuhusu ushiriki, kampeni hiyo inakuza uwezeshaji wa kifedha kwa kuhimiza Watanzania wengi zaidi kutumia benki kwa njia za kidigitali ambazo ni rahisi zaidi huku zawadi za pesa taslimu zikiwa na jumla ya mamilioni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...