Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali kupitia Kampuni ya Twiga Minerals imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kufanikisha mifumo ya sheria na utawala bora nchini.

Katika kufanikisha ajenda hiyo, Kampuni ya Barrick imekuwa mmoja wa wadhamini wa mafunzo kwa Mawakili wa serikali inayoendelea jijini Arusha ambapo imetunukiwa cheti cha udhamini.

Meneja wa Barrick nchini Dkt. Melkiory Ngido, akiongea na waandishi wa habari katika semina hiyo amesema kampuni ya Barrick nchini itaendelea kufanya kazi na Serikali kufanikisha uboreshaji wa mazingira ya kuboresha maisha ya wananchi katika sekta mbalimbali.

"Utawala wa kisheria ni moja ya suala la msingi katika uwekezaji ndio maana mafunzo haya kwetu tunaona ni muhimu ndio maana wakati wote tuko tayari kushirikiana na Serikali katika mchakato kama huu wa kutoa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali ikizingatiwa taasisi hii ni nyeti katika usimamizi wa raslimali za taifa ikiwemo sheria za uwekezaji na uendeshaji wa migodi", amesema Dkt. Ngido.
Meneja wa Barrick nchini Dkt. Melkiory Ngido.


Amesema kampuni ya Barrick nchini kupitia migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi imekuwa kinara wa kuchangia ukuzaji wa uchumi nchini kupitia kulipa Kodi na tozo mbalimbali za Serikali.


Ameeleza kuwa, pia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zinazotolewa na migodi yake zimefanikisha miradi mbalimbali katika maeneo yanayozunguka migodi hususani katika sekta za afya, elimu, maji na ujenzi wa miundombinu ya barabara.


Dk. Ngido amesema Barrick imeweza kuunga mkono jitihada za Serikali za kupanua wigo wa ajira kwa wananchi ambapo asilimia 96 ya wafanyakazi wake katika migodi ni Watanzania.


Aidha kampuni imekuwa kinara wa kutekeleza sera ya maudhui ya ndani (Local Content) ambapo asilimia kubwa ya wazabuni wake ni wazawa.


Mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa AICC yamefunguliwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Damas Ndumbaro.

Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Mawakili wa serikali jijini Arusha ambapo Kampuni ya Barrick imetunukiwa cheti cha udhamini.

Meneja wa Barrick nchini Dkt. Melkiory Ngido (kushoto) akiwa viongozi mbalimbali kwenye semina ya Mawakili wa Serikali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...