Mratibu Mkuu wa Malengo ya Maendeleo Endelevu - Fedha na Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Emmanuel Nnko ametoa wito kwa halmashauri nchini kubainisha vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitakuwa shirikishi na jumuishi vitakavyo wavutia wawekezaji katika halmashauri nchini ili kuondokana na utegemezi wa bajeti kutoka serikali kuu.
“Tumeendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo katika kuhakikisha tunapata njia mbadala za vyanzo vya mapato kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Hivyo, naomba nitoe wito kupitia mafunzo haya elekezi yakawe chachu ya kwenda kuratibu mipango mkakati yetu ya kupata vyanzo madhubuti vya mapato katika maeneo yetu”. Alisema Bw. Nnko na kuongeza “natambua utegemezi wa bajeti ya serikali kuu pekee hautoshi kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwani asilimia sitini na tano ya malengo haya kwa kiwango kikubwa yanafanyika kwenye serikali za mitaa”.
Wito huo umetolewa Jumatatu June 02, 2025 katika hafla ya kufungua Mafunzo ya Muongozo wa Upatikanaji wa Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa “Intergrated Local Financing Framework” (ILFF) unaojumuisha Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Makatibu Tawala Wasaidizi - Uchumi wa Mikoa ya Dodoma, Dar Es salama na Pwani pamoja na Wataalamu kutoka katika Halmashauri tatu za mfano ambazo ni Jiji la Dodoma, Manispaa ya Temeke, na Mji wa Kibaha.
Mafunzo haya yanayoratibiwa na Chuo cha Mipango kwa ufadhiri wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) yanafanyika katika Manispaa ya Morogoro.
Nae Mkurugenzi Msaidizi - Uratibu wa Shughuli za Serikali Idara ya Tawala za Mikoa Bw. Johnson L.K. Nyingi amesema kuwa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na Serikali wamekuwa na ushirikiano wa kihistoria katika kusukuma maendeleo nchini hivyo anaamini mafunzo haya yanayo ratibiwa na Chuo cha Mipango yanakwenda kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zikizikabili halmashauri zetu hususani kwenye vyanzo mbadala vya mapato.
“Nipende kuchukua fursa hii kuwashukuru sana Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa mchango inayotoa katika jamii yetu kwa ufadhili wa mafunzo haya na tathimini hii inayokwenda kufanyika katika halmashauri hizi za mfano, pia naomba kwa dhati kabisa kuwashukuru wataalamu wetu wa Chuo cha Mipango kwa kazi mnayoifanya. Ombi letu kwenu ni kuikamilisha kazi hii kwa kiwango na ufanisi mkubwa”. Alisema Bw. Nyingi.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mafunzo haya Dkt. Bonamax Mbasa amesema Chuo cha Mipango kitaendelea kutekeleza majukumu yake ya kutoa Ushauri Elekezi kwa kutatua changamoto mbali mbali za kimaendeleo katika jamii hususani katika ngazi ya serikali za mitaa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...