Usemi wa ombeni nanyi mtapewa, umedhihirisha usikivu wa Rais Samia Suluhu Hassan kupunguza gharama za lesini kwa maafisa usafirisha wa bodaboda, bajaji na guta zinazotumia umeme katika bajeti ya mwaka 2025-2026 kulipia kiasi cha shilingi elfu thelathini. 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa madereva guta za umeme yaliyofanyika katika chuo cha Polisi ikiwa ni mwezi mmoja toka atangaze maafisa hao wanahakikisha wanasajiliwa. 

Akizungumza na madereva wa guta za umeme, wakufunzi na viongozi wa shirikisho la maafisa hao Mpogolo amesema usikuvu wa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan umeendelea kuhakikisha vilio vya madereva wa vyombo vya moto vinasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi ili waweze kufanya shughuli zao kwa amani. 

Ameeleza kuwa kutolewa kwa mafunzo hayo na jeshi la polisi kutasaidia kuongeza uelewa na usalama, kutambulika rasmi kama familia kwa kusajiliwa tofauti na awali hawakuwa na leseni na hawakujulikana kwa urahisi. 

Katika mafunzo hayo, Mpogolo, amebainisha kuendelea kutoa ushirikiano kwa vijana walionufaika na mafunzo hayo kutoka maeneo mbalimbali kufanya shughuli zao vizuri katikati ya jiji kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu watazowekewa ili kupunguza msongamano katika masoko. 

Amesisitiza madereva wa maguta ya umeme, kufuata na kusimama katika sheria za barabarani kutokana na mafunzo waliyopata ili wanufaike kiuchumi kwa kujali muda wao na watumiaji wengine wa barabara. 

Mpogolo, ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha vijana kutumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi, ili waweze kusaidia familia zao na kutoa mchango wa maendeleo kwa serikali, kwa kuwa kazi ni msingi wa utu.

Na tayari jeshi la polisi limewafundisha misingi ya kazi yao , Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewasajili na kutambulika rasmi katika sekta ya usafirishaji, na  Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) imewapa leseni ili wafanye kazi kwa amani wakiwa barabarani.

Akizungumzia juu ya nishati safi, Mkuu huyo wa wilaya ya ilala, Edward Mpogolo, amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ni kinara namba moja wa kusisitiza matumizi ya nishati hiyo ni vema madereva wa maguta ya umeme kutumia vizuri fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa uaminifu,  usalama wa dereva, chombo chake, na kuwa na mahusiano mema kwani dunia ya sasa inafanya kazi kwa mtandao na wateja wanataka mizigo ifike haraka kwa kutumia usafiri ambao unatumia umeme. 

Aidha katika mafunzo hayo, Mpogolo ametoa shukrani kwa jeshi la polisi, wakiongozwa na Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Camillus Wambura, kwa kukubali ombi la kufanyika kwa mafunzo ya madereva maguta ya umeme kwa kupunguza gharama za masomo toka laki moja hadi elfu arobaini, na Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) kwa kutoa leseni. 

Kwa upande wao madereva maguta, katika risala yao  wameomba serikali iwasaidia kuangalia na kupunguza bei ya betri za maguta, maguta na  maeneo ya maegesho mjini.

Ombi ambalo, Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amelipokea na kuahidi kulifanyia kazi kwa kuhakikisha Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya atawapangia na wahakikishe wanafuata sheria, utaratibu na wasizibe njia na atatekaidi achukuliwe hatua. 

Huku akiwasisitiza kujiunga katika vikundi vya Saccos ya shirikisho,  kujisajili na kuomba mikopo ili waweze kupata mafanikio ya kazi zao kutokana na mikataba kandamizi.

Pamoja na kushughulikia suala la vipuri serikali itazungumza na kampuni zinazotengeneza maguta ya umeme waje kuwekeza nchini hali itayosaidia kuondoa madalali wa kati wanaoongeza bei za vifaa na kudhibiti upandishwaji wa bei. 

Mafunzo hayo yamefungwa kwa wahitimu wote kupatiwa vyeti, leseni na kuahidi kufuata sheria za usalama barabarani huku wakiwataka vijana wengine kwenda kupata mafunzo jambo litalosaidia kupunguza changamoto za kazi ya usafirishaji mizigo na vifurushi kwa haraka. 

Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni mwezi mmoja toka Mkuu wa wilaya ya ilala, Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya kukutana na madereva hao katika viwanja vya mnazi mmoja na kuwataka kusajiliwa ili watambulike rasmi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...