Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 100 kwa kukamilisha miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa mwaka 2020/2025.
Amesema hayo wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilala kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa kipindi cha miezi sita uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Karimjee Jijini humo.
Ametaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa ndani ya Wilaya kuwa ni ujenzi wa maghorofa nane ya shule za Sekondari yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 8 pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari Kitunda Relini wenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.6.
Akizungumzia sekta ya Afya Mkuu huyo wa Wilaya amesema Serikali imejipanga kujenga vituo vya afya kila kata huku akitolea mfano wa ujenzi wa Zahanati ya kisasa ya Mzinga pamoja na ununuzi wa vifaa tiba na madawa.
Aidha Mpogolo amesema katika kukuza na kuimarisha uchumi kwa Wananchi, Halmashauri ya Wilaya Ilala imeweza kutenga kiasi cha Shilingi bilioni 18 zitakazoanza kutolewa hivi karibuni kama mikopo isiyo na riba(mikopo ya asilimia 10).
"Uwezo wa Halmashauri yetu kwenye makusanyo umeongezeka, na kama uwezo umeimarika basi hata fedha tunazozitengakwa ajili ya miradi ya maendeleo hususan kwenye barabara tuongeze kutoka kwenye asilimia 10 kwenda asilimia 20".Alisema Mkuu huyo wa Wilaya
Mkutano huo maalum pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar e salaam Elihuruma Mabelya pamoja na wakuu wa Idara na vitengo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...