Na MWANDISHI WETU

DIWANI wa Kata ya Marumbo, Kisarawe, mkoani Pwani, Msafiri Mpendu, amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuifungua kata hiyo  kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano.

Ameyasema hayo alipowasilisha  taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Kata ya hiyo kwa mwaka wa fedha 2020 -2025 .

Diwani Mpendu, amesema   zaidi ya sh. milioni 227 zimepelekwa katika sekta ya afya kwenye miradi ya ujenzi wa zahanati, nyumba za watumishi na usambazaji wa mifumo ya maji.

Ameeleza, a katika  sekta ya elimu sh. milioni 239 zilipokelewa na kuelekezwa fedha  katika maendeleo ya miundombinu ya elimu  kama ujenzi wa madarasa, vyoo,majiko  na  ugawaji magodoro kwa wanafunzi.

Akizungumzia  sekta ya maji katika kata hiyo, Mpendu amesema wananchi wamenufaika na uchimbaji wa visima 16 vilivyochimbwa kimkakati.

 “Lengo ni  kuhakikisha visima hivi  vinahudumia idadi kubwa ya watu katika vijiji vyote vya kata hii ya Marumbo, kazi iliyofanywa na serikali pamoja na wadau,”amesema.

Kuhusu miundombinu ya  barabara, Mpendu, amebainisha ibainisha  uboreshaji huo umechochea  kiuchumi na kurahisisha upatikanajiwa huduma za kijamii.

Ameushukuru  Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)  kuhakikisha barabara muhimu zinapitika kwa urahisi katika misimu yote ya mwaka. 

Kuhusu huduma za kijamii Diwani  Mpendu, amesema hatua zinaendelea kuchukuliwa katika  mpango wa  kuimarisha lishe ambapo  katika kipindi cha miaka mitano  jumla ya ng'ombe 1400 walichinjwa.

“Tuligawa nyama kwa wananchi. Pia tuligawa vyakula mbalimbali katika  familia zenye mahitaji maalumu  kusaidia lishe  hasa kwa watoto,”amesema.

Amesema uwezeshaji huo ulifanywa ni diwani kwa kushirikiana na wafadhili.. 

Mpendu alisema  katika kuinua wanawake,vijana na watu wenye ulemavu  kiuchumi, serikali  chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan  ilitoa  kiasi cha sh. milioni 25 ambapo  vikundi vinne katika kata hiyo vimepata  mikopo  ya kuanzisha na kukuza biashara. 

“Kero ya mawasiliano katika kata hii imepatiwa ufumbuzi kwa  kuwekwa minara miwili ya kampuni za simu hali  iliyorahisisha mawasiliano na kufungua fursa ya kukuza uchumi, kurahisisha huduma za kutuma na kupokea fedha tofauti na awali,”ameeleza  Diwani Mpendu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...