Dar es Salaam, 20 Juni 2025
Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) wamesaini makubaliano mapya ya ushirikiano ili kuendeleza juhudi za kulinda na kuwapatia misaada ya kibinadamu wakimbizi na waomba hifadhi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanaoishi katika Kambi ya Nyarugusu, pamoja na wale wapya wanaopokelewa katika Kituo cha mpito mkoani Kigoma, Tanzania.
Kupitia mchango wa shilingi bilioni 9.2 (sawa na EUR milioni 3), Umoja wa Ulaya unaunga mkono jitihada za UNHCR za kutoa msaada wa haraka wa kuokoa maisha na huduma muhimu kwa mahitaji ya ulinzi katika sekta za mbalimbali ikiwemo afya, maji na usafi wa mazingira (WASH), makazi na elimu — zikiwemo huduma maalum kwa watu wenye mahitaji ya kipekee waliokimbia machafuko kutoka DRC.
“Kuongezeka kwa migogoro duniani kumesababisha idadi kubwa ya wakimbizi wanaohitaji msaada wa
haraka. Ndiyo maana leo ninajivunia kutangaza usainishwaji wa mkataba wa shilingi bilioni 9.2 (EUR milioni 3) na UNHCR hapa Tanzania. Makubaliano haya muhimu yatanufaisha moja kwa moja wakimbizi walioko nchini, kwa kuhakikisha ulinzi wao, kuwasaidia kuishi maisha ya heshima, na kuwawezesha kupata njia za kujikimu.
Kama Umoja wa Ulaya, tunaendelea kushikilia misingi ya ubinadamu na mshikamano wa kimataifa.
Ni lazima tuendelee kushirikiana kukabiliana na changamoto hizi za kimataifa na kulinda haki na utu wa kila mtu anayetafuta hifadhi,” amesema Balozi Christine Grau, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwaka 2025, UNHCR kwa kushirikiana na wadau wa kitaifa na wa kimataifa, inaendelea kuiunga mkono
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupokea waomba hifadhi wapya wanaowasili mkoani Kigoma Kutoka DRC. Kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu, zaidi ya waomba hifadhi 3,000 wamepokelewa Kigoma.
Wakati huo huo, UNHCR na wadau wanaendelea kutoa huduma kwa wakimbizi wa Kongo wapatao
85,105 walioko katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. Wakimbizi hawa hupokea msaada wa haraka
ikiwemo malazi salama, chakula, huduma za afya, maji safi, miundombinu ya usafi wa mazingira, pamoja na huduma nyingine muhimu.
Kutokana na hali ya taharuki inayowalazimu wakimbizi kukimbia makazi yao — mara nyingi hufanikiwa
kuondoka na nguo walizovaa tu na mali chache wanazoweza kubeba — upatikanaji wa huduma za afya,
malazi, maji safi, usafi na mazingira salama ni muhimu sana. Huduma hizi hupunguza vifo na magonjwa, lakini pia hulinda utu, usalama, na ustawi wa jumla wa wakimbizi na waomba hifadhi.
“Kuhudumia wakimbizi na waomba hifadhi kutoka Kongo walioko Tanzania si wajibu tu — ni taswira ya
ubinadamu wetu wa pamoja. Kupitia msaada madhubuti kutoka kwa washirika kama Umoja wa Ulaya,
hatutoi tu huduma za haraka, bali tunawekeza katika utu, ustahimilivu, na misingi ya amani ya kudumu kwa familia zinazostahili matumaini na mustakabali bora,” amesema Zulqarnain Hussain Anjum, Mwakilishi wa UNHCR a.i. nchini Tanzania.
UNHCR inahitaji takribani Dola za Kimarekani milioni 14 (sawa na shilingi bilioni 37.8) kukabiliana na dharura ya wakimbizi wa DRC nchini Tanzania, ikiwemo Dola milioni 5 (shilingi bilioni 13.5) kwa ajili ya maandalizi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...