Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.Salvator Chuwa ,akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20,2025 jijini Dodoma kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

....

TUME ya Ushindani (FCC) imependekeza kuanzishwa kwa kozi maalum katika vyuo vya elimu ya juu nchini itakayolenga kuwajengea vijana uwezo wa kitaalamu wa kutambua na kupambana na bidhaa bandia, ikiwa ni mkakati wa muda mrefu wa kulinda walaji na soko la haki.

Hayo yamesemwa leo Juni 20,2025 jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.Salvator Chuwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Aidha Chuwa, amesema elimu kwa umma ndio silaha madhubuti ya kupambana na biashara ya bidhaa bandia, na kwamba vijana wa vyuoni wanapaswa kupewa nafasi ya kuwa mabalozi wa mabadiliko katika jamii kupitia elimu hiyo.

“Tumeendelea kushirikiana na vyuo vikuu kama SUA, UDOM, UDSM, Mzumbe, St. Augustine, MUST na vingine kwa kutoa semina juu ya athari za bidhaa bandia. Tunashauri elimu hiyo sasa iende kuwa sehemu ya mitaala ya kudumu ya vyuo,” amesema Chuwa

Amesema lengo ni kuhakikisha kuwa taifa linajenga kizazi kinachoelewa thamani ya miliki bunifu, haki za watumiaji na madhara ya bidhaa bandia kiuchumi na kiafya. “Tunataka vijana waelimike kabla ya kuwa waathirika au wadau wa mifumo inayohalalisha bidhaa haramu,” anasisitiza.

FCC imekuwa ikitoa elimu kwa makundi mbalimbali ikiwemo Wakuu wa Mikoa, wabunge, wajasiriamali, vyombo vya habari, na wafanyabiashara wa Kariakoo, kupitia semina, warsha na makongamano.

Ngasongwa amesema elimu hiyo imeongeza ushirikiano baina ya FCC na taasisi kama ZFCC (Zanzibar), ACA (Kenya) pamoja na Chama cha Wakala wa Forodha (TAFA), katika mapambano ya kimkakati ya kikanda dhidi ya bidhaa bandia.

Aidha, amesema wito huo unakwenda sambamba na juhudi za kitaifa katika kukuza uchumi wa ubunifu na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika Soko Huru la Biashara Afrika (AfCFTA), ambalo linahitaji bidhaa bora na halali kutoka kila nchi mwanachama.

FCC imetoa rai kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana na vyuo husika kutathmini uwezekano wa kuanzishwa kwa moduli au mtaala maalum wa “Uchunguzi wa Ubora na Uhalisia wa Bidhaa” kwa ngazi ya stashahada na shahada.

Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani kitaadhimishwa Juni 25, 2025 katika Ukumbi wa Mabeo, jijini Dodoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,ambapo vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini watashiriki kupitia mijadala na maonyesho ya ubunifu wa bidhaa halali.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.Salvator Chuwa ,akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20,2025 jijini Dodoma kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.Salvator Chuwa ,akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20,2025 jijini Dodoma kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.Salvator Chuwa ,akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20,2025 jijini Dodoma kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...