Mbinga-Ruvuma.

Halimashauri ya Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma,imekufanikiwa kukusanya Sh.bilioni 12.2 kati ya lengo la awali la kukusanya Sh.bilioni 8.4 hadi kufikia tarehe 30 Juni 2025.

Akitoa taarifa kwenye kikao maalum cha Baraza la madiwani la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Mkuu wa kitengo cha fedha na Uhasibu Halmashauri hiyo CPA Samwel Marwa alisema,katika kipindi cha miaka minne mapato ya yameongezeka kutoka Sh.bilioni 3.4 mwaka 2021 hadi kufikia Sh.bilioni 12.4.

Alisema,kuongezeka kwa mapato hayo kunatokana na ushirikiano mkubwa wa wataalam wa Halmashauri,madiwani na wananchi,kuzingatia sheria ndogo za Halmashauri na usimamizi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato.

Aidha,alitaja vyanzo vikuu vya mapato ni  ushuru wa zao la kahawa lililochangia Sh.bilioni 4.3,makaa ya mawe Sh.bilioni 3.3,ushuru wa huduma Sh.bilioni 1.35, zao la mahindi Sh.867,wananchi kwenye ngazi ya kata Sh.677 na vyanzo vingine sh.bilioni 5.183.

Kwa mujibu wa Marwa,katika utekelezaji wa majukumu ya ukusanyaji wa mapato changamoto kubwa ni rasilimali  ya magari kwani yaliyopo ni machachena baadhi ya wananchi kutopenda kulipa kodi za serikali.

“ hata hivyo katika kukabiliana na changamoto zlizopo Halmashauri inalazimika kutumia magari machache tuliyonayo kwa mfano asubuhi yanakwenda kufanya kazi nyingine na jioni tunayatumia kwa ajili ya kukusanya mapato,kwenye makaa ya mawe tunafanya ulinganifu kwenye geti kuu la Kitai,kuchukua hesabu za tume ya madini na tumeanzisha kituo cha ukaguzi  wa magari yanayobe makaa kwenye kwenye mizani eneo la Lipokela”alisema CPA Marwa.

Kuhusu hoja zilizoibuliwa kwenye ukaguzi wa Hesabu za Serikali alisema,hoja za zamani zilikuwa 10,zilizofanyiwa kazi 3 bado 7 na  mwaka wa fedha 2023/2024 hoja zipo 31 zilizofanyiwa kazi 11 bado 20 na maagizo ya LAAC yalikuwa 4 yaliyofanyiwa kazi 1 bado 3.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo,aliipongeza Halmashauri hiyo kwa mafanikio hayo na kupata hati safi katika ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

“Mheshimiwa Mwenyekiti natambua kuwa Halmashauri yenu  imepata hati safi,nawapongeza sana kwa jitihada zenu ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kupata matokeo haya chanya”alisema Makondo.

Makondo,amewataka watumishi na wataalam wa Halmashauri ya Mbinga kuendeleza nidhamu na uwajibikaji kwa sababu mafanikio hayo ni ushaihidi wa usimamizi thabiti wa sheria na miongozo ya Serikali.

Alisema,kupata hati safi si kazi rahisi,lakini kuendelea kuipata kila mwaka kunahitaji sana kujituma zaidi na kipimo cha utendaji kazi nzuri kwa Halmashauri yoyote ni uwezo wake wa kukusanya mapato yake ya ndani.

Makondo,ameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha inatumia mfumo wa kisasa wa ukusanyaji mapato TAUSI katika kujibu hoja za CAG na maagizo ya kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa(LAAC).

Awali Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Ruvuma Nicolas Kilinga,ameitaka Halmashauri hiyo kupunguza kujibu hoja zilizoibuliwa kwenye ukaguzi na kujibu maagizo ya LAAC haraka ili kuzuia kuongezeka kwa hoja kwa mwaka mwingine wa fedha 2025/2026.

“ili kuzuia kuzalisha hoja mpya ni vema kumtumia mkaguzi wenu wa ndani wa Halmashauri ambaye atapitia taarifa zenu kabla ya kuja Mkaguzi wa nje,wakuu wa idara na vitengo mshiriki  kikamilifu kutafuta majibu ya hoja mnazotakiwa kuzijibu”alisema Kilinga.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...