Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura akikata utepe kuzindua rasmi jengo jipya la kisasa la Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto mjini Tarime, Mara. Jengo hilo limejengwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kupitia Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili wa Serikali ya Finland, chini ya Programu ya Chaguo Langu Haki Yangu.



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura (kushoto), akikagua chumba cha mikutano ndani ya jengo hilo.

Mratibu wa TGNP, Flora Ndaba akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo

Na Mwandishi Wetu, Tarime


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, leo Juni 24, 2025 amezindua rasmi jengo jipya la kisasa la Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto mjini Tarime, Mara.


Jengo hilo limejengwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kupitia Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili wa Serikali ya Finland, chini ya Programu ya Chaguo Langu Haki Yangu.


Katika hotuba yake, IGP Wambura amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kujenga mahusiano na mataifa mbalimbali, likiwemo la Finland.

“Jengo hili litakuwa kimbilio salama la wahanga wa ukatili wa kijinsia,” amesema IGP Wambura na kuwapongeza UNFPA, TGNP na Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, Mark Njera, kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo hilo.


Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote kupiga vita ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji, akisema “Vita dhidi ya ukatili wa kijinsia siyo suala la familia pekee, bali ni la jamii nzima.”


Kwa upande wake, Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii nchini (CP), Faustine Chilogile, amesema uzinduzi wa jengo hilo umetanguliwa na elimu ya ukatili wa kijinsia na madhara yake katika kata 60 za Mkoa wa Polisi Tarime Rorya.


Naye Dkt. Majaliwa Gerald Marwa kutoka UNFPA Tanzania, amesema ujenzi wa jengo hilo la Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto ni uthibitisho wa dhamira ya serikali na wadau ya kulinda watu dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.


Mratibu wa TGNP, Flora Ndaba, amesema ujenzi wa jengo hilo umegharimu shilingi milioni 300, na kwamba jingine kama hilo limejengwa Unguja, Zanzibar.


Hafla ya uzinduzi wa jengo hilo pia imehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Meja Edward Gowele (Tarime) na Dkt. Khalfan Haule (Rorya), miongoni mwa viongozi wengine wa serikali, dini na chama tawala - CCM.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...