MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amesema kazi iliyobaki baada ya kuvunja Bunge ni kuendesha taratibu za namna ya kupata wagombea ubunge na kwamba Chama hicho hakitaka mgombea ila kitateua mmoja kati ya wengi.

Wasira ameyasema hayo leo Juni 24,2025 alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wakati kihitimisha ziara yake katika mkoa huo..

“Kazi iliyobaki kwa CCM baada ya kuvunja Bunge ni kuendesha taratibu za namna ya kupata wagombea ubunge na sisi tumesema wanachama wetu wanaotaka ubunge wako wengi lakini sisi tunataka mgombea mmoja kwa kila jimbo.

“Sasa tumesema wagombea wengi lakini tutajucha na wala hatuwakati tunateua , unajua tofauti ya kuteua na kukata? Ukikata unakata kwa hasira ukiteua unatazama uwezo kwa wakati”

Aliongeza kwahiyo wao hawakati mtu ila wanateua wagombea wachache kati ya wanachama wengi wale wanaobaki watasubiri tena ,wengine ni vijana watasubiri.

“Wanajua Juni 28 wanagombea  wanaleta fomu, Julai 2 wanarudisha fomu kwa heshima tu halafu wakimaliza vikao vyetu vitawatizama tazama na kupendekeza na tunataka kupendekeza wagombea ambao wanakubalika na wananchi.”









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...