*Aelezwa kuhusu majukumu yanayotekelezwa na kupongeza

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (UTUMISHI), Juma Mkomi, ametembelea banda la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma na kukagua maandalizi yake.

Akiwa na viongozi wengine kutoka katika ofisi hiyo ya Rais (UTUMISHI) miongoni mwao akiwa ni Mkurugenzi Benard Makhanda na Mkurugenzi Msaidizi Jafari Maganga, Katibu Mkuu amepongeza maandalizi ya banda hilo na kusikiliza maelezo kuhusu majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na NCC.

Katika maelezo hayo yaliyotolewa na Afisa Habari na Uhusiano Mkuu wa NCC, Bi. Namsembaeli Mduma, Katibu Mkuu alielezwa baadhi ya majukumu hayo kuwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu, uratibu wa usuluhishi wa migogoro inayohusu sekta ya ujenzi na uandaaji wa fahirisi ya bei ya vifaa vya ujenzi.

Majukumu mengine ni kuratibu na kufanya utafiti, ukaguzi wa kiufundi wa miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa nchini, kutoa mafunzo yakuwajengea uwezo wadau wa sekta ya ujenzi, wakiwemo wahandisi, wakadiriaji majenzi, wabunifu majengo na wengine kutoka katika sekta mbalimbali.

Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16, mwaka huu, itazinduliwa rasmi kesho na kuhitimishwa Juni 23, mwaka huu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi, akiingia kwenye Banda la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC).

Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Jafari Maganga akisaini kitabu cha wageni katika Banda la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) baada ya kusikia maelezo kuhusu Baraza hilo. Bw.Maganga ni miongoni mwa viongozi walioambatana na Katibu Mkuu wa UTUMISHI kutembelea banda hilo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , Bw. Juma Mkomi akipewa maelezo na Ofisa Habari na Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi  (NCC), Bi. Namsembaeli Mduma, kuhusu majukumu ya Baraza hilo wakati alipotembelea banda la NCC akiwa na viongozi wengine kutoka katika ofisi yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...