NA MWANDISHI WETU, VUNJO.
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Charles Stephen Kimei, leo mchana amerejesha rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania tena ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ofisi za chama Wilaya ya Moshi Vijijini.
Katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi (2020–2025), Dkt. Kimei amefanikisha kwa kiwango cha juu utekelezaji wa Ilani ya CCM, ikiwemo Shilingi Bilioni 52 za miradi ya maendeleo, Ujenzi wa vituo vya afya 4 na zahanati 12
Miradi mingine aliyotekeleza ni miradi ya maji safi, iliyopelekea upatikanaji kuongezeka kutoka asilimia 44 hadi 79 vijijini na 82 mjini, ujenzi wa shule 4 za sekondari na 1 ya msingi, ufikishaji wa umeme katika vitongoji 151 kati ya 191na maboresho ya barabara na miundombinu ya umwagiliaji
Haya ni mafanikio yanayoelezwa na wananchi wengi kuwa na nafasi ya kipekee ya kumrudisha kwa kipindi cha pili ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya jimbo hilo kwa zaidi ya miongo miwili.
Mpaka sasa, zaidi ya wagombea wanane (8) wamechukua na kurejesha fomu za kuomba uteuzi ndani ya CCM kwa Jimbo la Vunjo, ishara ya wazi ya ushindani wa kidemokrasia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...