Na Janeth Raphael MichuziTv -Bungeni Dodoma

MBUNGE wa Kilwa Kaskazini,Francis Ndulane (CCM) ameshauri mambo sita kwa Wizara ya Afya ikiwemo kupeleka Huduma za kupima magonjwa mbalimbali kwa kutumia Mashine za kisasa za CT Scan na MRI katika ngazi za Mikoa na wilaya.

Akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya leo Julai 3,2025 bungeni,Mbunge huyo amesema vifaa vya CT Scan na MRA vimekuwa vikipatikana katika hospitali za Kanda pekee huku baadhi ya hospitali za Mikoa zikosa.

“Leo wananchi wengi wanahangaika kuna hospitali za wilaya hakuna vifaa hivi hebu, Serikali iangalie hili jambo ili waweze kutulia tuweke CT Scan mpaka Wilayani ili tuwatibu wananchi wetu,”amesema Mbunge huyo

Pia, Mbunge huyo amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya kutokuwepo kwa mashine za kupimia damu katika hospitali za wilaya kwa wagonjwa wa figo hali ambayo imekuwa ikiwapata wakati mgumu wagonjwa.

Amesema kuna haja ya huduma hizo zitolewe bure kama inavyofanya kwenye kifua kikuu na saratani kwani wengi wamekuwa na changamoto.

Aidha ameshauri kuangaliwa upya vifurushi vya NHIF kwani wananchi wenye kipato cha chini baadhi wamekuwa wakishindwa kutokana na kutokuwa na fedha.

“Nilikuwa naomba kwa wazee tusifike mahali wakatuona ni kundi ambalo limepata laana ama au kama hatuwataki,wazee wanatibiwa kwa gharama kubwa hili waliangalie ikiwezekana mfuko NHIF upewe nafuu fulani ili uwasaidia wazee kwani wamelitumikia Taifa na kuzalisha kwa muda mrefu tutakuwa tumewasaidia sana,”amehoji Mbunge huyo.

Aidha ameshauri pia suala la matumizi ya tehama katika huduma za afya ili kuondoa wizi katika mapato na kuweza kuiongezea mapato serikali.

Pia ameshauri Wizara kuweka mkazo katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili watanzania waweze kupata huduma hizo kwa urahisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...