NA. MWANDISHI WETU – GENEVA USWISI
TANZANIA imeshiriki Jukwaa la Nane la Dunia la Kupunguza Madhara ya Maafa lenye jukumu muhimu katika kuhamasisha na kukuza ushirikiano kati ya Serikali, Wadau na Mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kuharakisha utekelezaji wa hatua za kupunguza madhara ya maafa.
Akizungumza wakati wa Mkutano huyo unaoendelea Mjini Geneva Uswisi kuanzia tarehe 02 hadi 6 Juni 2025, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri, Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt.Jim Yonazi alisema jukwaa hilo ni chombo cha kutathmini, kujadili maendeleo ya utekelezaji na kuimarisha masuala ya usimamizi wa maafa kimataifa kupitia makubaliano ya hiyari ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo yameridhiwa na Makubaliano ya hiyari ya kimataifa yanayotekelezwa kwa sasa ni Mkakati wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafa 2015 – 2030.
“Jukwaa hili hutumika kama chombo muhimu cha kukuza ushirikiano katika utekelezaji wa ajenda nyingine za kimataifa zinazochangia kupunguza madhara ya maafa, ikiwa ni pamoja na mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi na malengo ya maendeleo endelevu.
Aliongeza kuwa, Matokeo ya jukwaa hilo yanatumika katika kutoa muelekeo wa masuala ya usimamizi wa maafa katika maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, baraza la umoja wa mataifa la kiuchumi na kijamii na jukwaa kuu la kisiasa la umoja wa mataifa kuhusu maendeleo endelevu.
Kwa mujibu wa Dkt. Yonazi ameelezwa kuwa, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa imepewa jukumu la kuandaa Jukwaa la Dunia na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Jukwaa hufanyika kila baada ya miaka miwili ambapo tangu mwaka 2007, limefanyika mara saba.
Vilevile alisema jukwaa hilo limejumuisha ajenda kuhusu kuimarisha utekelezaji wa mkakati wa Sendai kwa kuzingatia maendeleo na changamoto zilizoainishwa katika mapitio yake ya muda wa kati na Azimio lake kupitia Baraza la Umoja wa Mataifa 2023,
Ajenda nyingine ilihusu kuimarisha mikakati ya kitaifa na serikali za mitaa na mipango ya kupunguza madhara ya maafa, kwa kuzingatia athari za maafa ya hivi karibuni;
“Jukwaa limejadili namna ya kuimarisha mitandao iliyopo na kuanzisha ushirikiano mpya katika ngazi za kimataifa, kitaifa na wadau wa ndani, kubadilishana ujuzi, teknolojia na uzoefu kuhusu sera, programu na uwekezaji kuhusu kupunguza hatari ya maafa.
Dk.Yonazi alisema matokeo ya ushiriki wa jukwaa hilo ni kuimarisha utekelezaji wa Mkakati wa Sendai kupitia Sheria na Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa kwa kupata uzoefu na fursa za kimataifa na wadau.
Matokeo mengine ni kuimarisha uratibu na ushiriki wa pamoja wa sekta na mtazamo wa wadau katika kutekeleza shughuli za maeneo ya maendeleo endelevu, kuibua fursa za rasilimali fedha na mipango ya kiuchumi, kuimarisha miundombinu, hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda mifumo wa ikolojia katika maeneo ya kupunguza hatari ya maafa, tahadhari ya mapema na kurejesha hali.
“Jukwa hili litasaidia kuongeza uwekezaji katika usimamizi wa maafa na tahadhari ya mapema kwa wote kupitia ushirikiano na taasisi za Umoja wa Mataifa na Kimataifa,”alisema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...