Hali ya joto la kisiasa katika mtanange wa mbio za Ubunge katika Jimbo jipya la Kivule Mkoani Dear es Salaam, imeanza kupanda, baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Komredi Brendan Maro, pichani kulia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, kujitosa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo hilo jipya.

Komredi Maro anakumbukwa kwa jitihada zake za kuwaunganisha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (Umma na Sekta Binafsi) Katika kutekeleza wajibu wao kwa waajiri, lakini pia katika kujenga hoja za kulindwa kwa Utu, haki na maslahi ya wafanyakazi.

Pamoja na nafasi hizo, Komredi Maro amewahi kuhudumu pia kama Mwenyekiti wa Mkoa wa Shirisho la Vyama huru vya Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Dar es Salaam, ambako anakumbukwa kwa kushiriki kikamilifu Katika hoja za maboresho ya Sheria na Kanuni za mafao (Kikotoo), huku akifanikiwa kuwaunganisha na kuwashawishi Wafanyakazi kuendelea kuwa watulivu na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, akiwahakikishia TUCTA inaendelea na majadiliano na Serikali Katika kutafuta mwafaka.

Hivi Karibuni, kupitia Sherehe za MeiMosi, Mhe.Rais *Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitangaza maboresho ya Kanuni hiyo na kupandisha kima cha chini cha mshahara na nyongeza ya mshahara kwa Watumishi wa Umma, kama matokeo ya majadiliano baina ya Serikali na TUCTA.

Komredi Maro, ambaye ni Mkazi wa Kata ya Kitunda, Jimboni Kivule, anatajwa kuwa mmoja kati ya vijana wasomi waliolelewa katika Chama cha Mapinduzi, aliyeshiriki katika kampeni mbalimbali za chama, wenye upeo na uwezo wa uchambuzi, kujenga hoja na kutoa ushawishi kwa watu, sifa zinazopelekea aonekane kuwa mmoja wa watu sahihi sana kwa changamoto za Jimbo la Kivule.

Aidha, kawaida yake ya ushirikiano siyo tu na viongozi wenzake lakini pia na watu anaowaongoza inatajwa kuwa turufu muhimu kwake Katinka mbio hizo.

Hata hivyo, licha ya uwezo wake wa kuimudu nafasi hiyo, changamoto inayoweza kumkabili ni kuwa mtu aliyetokea kwenye Familia ya kawaida kabisa kiuchumi, hali inayoweza kukwamisha mpambano wake mbele ya watia nia wenye uchumi mkubwa.

Juhudi za kumpata ili kuelezea jinsi alivyojiandaa na mpambano huu hazikuzaa matunda, baada ya kujibu kwa ufupi kuwa "Chama chetu na Wanakivule wenyewe wanakijua wanachokitaka na namna ya kukipata."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...