Picha ya pamoja mara baada ya kutoa Mafunzo ya Maktaba Maktaba na mtandao.
Afisa Maktaba Elias Ntobi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe akizungumza wakati akitoa elimu ya Maktaba na aina zake na namna ya kuzitumia kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kijitonyama Sayansi iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Juni 3, 2025.
Dar es Salaam, Juni 3, 2025.
CHUO Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam, leo wametoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kijitonyama kuhusu umuhimu wa kutumia maktaba pamoja na maktaba mtandao.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Maktaba Elias Ntobi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe alisema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuhakikisha kila mwanafunzi anafahamu aina mbalimbali za maktaba na namna bora ya kuzitumia katika kujifunza.
“Kupitia mafunzo haya, tunalenga kuwawezesha wanafunzi kufahamu umuhimu wa maktaba, hususan maktaba mtandao ambayo ni rahisi kutumia kupitia vifaa vya kielektroniki kama simu janja na kompyuta,” alisema Ntobi.
Ameongeza kuwa maktaba mtandao huwapa wanafunzi fursa ya kupata taarifa mbalimbali za kielimu kwa urahisi zaidi, jambo litakalowawezesha kuongeza maarifa na ujuzi muhimu katika masomo yao ya kila siku.
Ntobi pia alibainisha kuwa elimu hiyo itasaidia wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao kwa kutumia vitabu na nyenzo nyingine za kujifunzia.
Afisa Maktaba kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Benard Msengi, alieleza kuwa maktaba mtandao inatoa fursa kwa wanafunzi kusoma mahali popote bila kulazimika kufika kwenye jengo la maktaba. “Tumewapatia pia kiambatanisho kitakachowasaidia kuangalia masomo pamoja na mitihani ya nyuma, na wanaweza kujiunga moja kwa moja na maktaba mtandao ili waendelee kujifunza zaidi,” alisema.
Elimu hii ni sehemu ya juhudi za Chuo Kikuu Mzumbe kuendeleza jamii kwa njia ya maarifa, huku wakisisitiza umuhimu wa teknolojia katika kuboresha elimu kwa wanafunzi wa ngazi zote..Aidha Ntobi aliwapa mbinu mbali za kupenda kujisomea ( Reading habitual)kwa kwa kupenda kusoma sio tu kutawasaidia katika elimu yao lakini watakuwa na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi sahihi (Right decision) katika maisha yao kwani jamiii iliyo na taarifa za kutosha (Well informed society) ni jamii iliyostarabika.
Baada ya Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam, kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya maktaba na maktaba mtandao kwa wanafunzi wa Shule hiyo ya Kijitonyama Sayansi, walimu wameonyesha shukrani na kufurahishwa na elimu waliyoipokea.
Mwalimu wa shule hiyo, Rukia Butenge, ameishukuru Mzumbe kwa hatua hiyo muhimu akisema: “Nimefurahia sana ujumbe kutoka Chuo Kikuu Mzumbe. Wametufundisha kwa kina kuhusu maktaba mtandao, na kwa kweli tumepata maarifa mapya ambayo hapo awali hatukuwa tunayafahamu vizuri.”
Rukia mbali na kuwashukuru wawezeshaji kwa mafunzo waliyotoa mwalimu huyo amesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia wanafunzi kupanua uwezo wao wa kufikiri na kujifunza kwa kujitegemea: “Wanafunzi wetu sasa wataweza kujiongeza kufanya vitu kwa ufanisi hata bila uangalizi wa walimu. Nawapongeza Mzumbe kwa juhudi hizi, na nawasihi waendelee kutembelea shule nyingine ili na wanafunzi wengine wanufaike."
Bw. Fred Kivike Mkutubi Msaidizi licha ya kuwafundisha kuhusu matumizi ya maktaba wanafunzi hao alipata nafasi ya kufahamishwa kozi mbalimbali zinazofundishwa Chuo Kikuu Mzumbe kwa na kuwakaribisha kwa kuja kusoma Mzumbe Chuo Kikuu.
Miongoni wa wanafunzi waliofaidika na elimu hiyo ni Diana Pashenzi wa kidato cha tatu na Fadi Maketa wa kidato cha kwanza ambao kwa pamoja wamesema awali hawakuwa na ufahamu kuwa wangeweza kutumia simu kutafta simu ambazo zinngewasaidia kutafita aarifa ambazo zingiwasaidia katika masomo yao walitumia simu kucheza gamu na kuangalia taarifa nyingine hasa za burudani.
Chuo Kikuu Mzumbe kimekuwa na utamaduni wa kushiriki kikamilifu katika utoaji wa huduma kwa jamii, ikiwa ni sehemu ya utekeleza Mpango Mkakati wa Chuo hicho.


Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kijitonyama Sayansi Rukia Butenge akizungumza wakati Chuo Kikuu Mzumbe wakitoa elimu ya Maktaba mtandao namna ya kutumia kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kijitonyama Sayansi iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Juni 3, 2025.
Fred Kivike Mkutubi Msaidizi akizungumza wakati akikitangaza chuo Kikuu Mzumbe kwa Ujumla.
.jpeg)

Matukio mbalimbali katika picha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...