NA EMMANUEL MBATILO, KIBAHA

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kupitia Kituo chake cha Umahiri wa Usalama Barabarani, kwa kushirikiana na Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la polisi, kimeendesha mafunzo maalum kwa maafisa usafirishaji wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

Mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa wa sheria na taratibu za usalama barabarani kwa wadau mbalimbali wa usafirishaji, wakiwemo waendesha bodaboda na madereva wa magari ya abiria, ili kuchangia juhudi za kupunguza ajali za barabarani na kuokoa maisha ya wananchi.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa Kituo cha Kikanda cha Umahiri katika Usalama Barabarani kutoka NIT, Godlisten Msumanje, aliwataka madereva kuzingatia kikamilifu sheria za usalama barabarani kama njia ya kujilinda wao na abiria wao.

“Madereva wa bodaboda wanapaswa kuvaa kofia ngumu kila wakati na kuepuka kupakia abiria zaidi ya mmoja. Hii ni kwa usalama wao na wa abiria wao pia,” amesema Msumanje.

Kwa upande wao, Abbas Mizambwa, Msaidizi wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kibaha Mjini, pamoja na Mkaguzi wa Polisi Happiness Mndeme kutoka dawati la Elimu ya Usalama Barabarani, wamesema elimu hiyo ni muhimu kwa madereva wote, hasa vijana ambao wengi wao huendesha bila mafunzo rasmi ya udereva.

“Madereva wa bodaboda wanapaswa kuvaa kofia ngumu kila wakati na kuepuka kabisa tabia ya kupakia abiria zaidi ya mmoja, hii ni kwa usalama wao na wa abiria wao pia,” amesema Msumanje.

Kwa upande wao, Msaidizi wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kibaha Mjini, Abbas Mizambwa, pamoja na Mkaguzi wa Polisi kutoka dawati la Elimu ya Usalama Barabarani, Happiness Mndeme, wamesema elimu hiyo ni muhimu kwa madereva hasa vijana wanaoendesha bodaboda ambao wengi hawajapata mafunzo rasmi ya udereva.

“Lazima tuhamasishe vijana kusomea fani ya udereva badala ya kuingia barabarani bila maandalizi ya kutosha hii ndiyo njia pekee ya kupunguza ajali,” alisema Mizambwa.

“Tunaendelea kutoa elimu ya mara kwa mara kwa kushirikiana na wadau kama NIT ili kuhakikisha kila dereva anakuwa na uelewa wa kutosha wa usalama barabarani.”ameongeza Mndeme

Nae Katibu wa Bodaboda wa Kata ya Mkuza, Daudi Masalu amesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kubadili fikra za madereva kuhusu wajibu wao barabarani nakupongeza NIT elimu kwa madereva na kuomba elimu hiyo iwe endelevu.

“Tunajifunza mengi tunayoyadharau kwenye kazi ya kila siku. tukifundishwa mara kwa mara, ajali zitapungua,” amesema Masalu.

Naye Ahmad Kanyenyela, Afisa Usafirishaji wa daladala, ameongeza kuwa mafunzo hayo yanapaswa kupewa msukumo mkubwa kwa sababu madereva wengi wanahitaji ujuzi na maarifa ya kitaalamu ili kuwa salama barabarani.

Kwa mujibu wa takwimu za Jeshi la Polisi, watu 1,275 wamepoteza maisha kati ya Januari hadi Aprili mwaka huu kutokana na ajali za barabarani nchini. Hali hiyo inadhihirisha umuhimu wa kuwekeza zaidi katika elimu ya usalama barabarani na udhibiti wa nidhamu miongoni mwa madereva ili kuokoa maisha ya Watanzania.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...