Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Dkt. Christopher Timbuka, amesema mafanikio ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) yanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika jitihada za kitaifa za uhifadhi wa mazingira, hasa katika kipindi ambacho Serikali ya Awamu ya Sita inaelekeza nguvu kubwa katika utunzaji wa vyanzo vya maji, kupanda miti na kuimarisha mapato yasiyoharibu ikolojia.
Dkt. Timbuka aliyasema hayo Juni 24, 2025, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa TFS walipotembelea ofisi yake katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa majukumu ya wakala huo na kutathmini mchango wake katika uhifadhi na maendeleo ya jamii.
Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Timbuka aliipongeza TFS kwa ushirikiano mzuri na ofisi yake na kueleza kuwa wakala huo umeonesha mafanikio makubwa katika kusaidia taasisi na wananchi kupunguza utegemezi wa misitu kwa matumizi yasiyoendelevu.
“TFS wamekuwa wakisambaza miche ya miti kwa taasisi na wananchi, wakihamasisha upandaji wa miti na kutoa elimu ya mazingira. Hii inasaidia kupunguza matukio ya moto na uharibifu wa misitu kwa sababu wananchi wanajua thamani ya kuilinda,” alisema Dkt. Timbuka.
Aliongeza kuwa wilaya hiyo imeanza kuona mafanikio ya jitihada hizo, ikiwemo kupungua kwa matukio ya moto wa misitu na kuongezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuitunza miti waliyoipanda, tofauti na awali ambapo miti ilipandwa kwa ajili ya sherehe na kupigwa picha pekee.
“Tunasisitiza kuwa utunzaji wa miti ni muhimu kuliko kupanda tu. Leo miche mingi inaliwa na mifugo, tunawahamasisha wananchi waelewe kuwa miti inahitaji uangalizi ili ikue. Wapo wanaoelewa, wengine bado, lakini sisi kama viongozi tutazidi kuwahamasisha,” aliongeza.
Katika kuimarisha motisha ya wananchi kushiriki uhifadhi, Dkt. Timbuka aliipongeza TFS kwa kuanzisha miradi ya asali kupitia ufugaji wa nyuki ndani ya misitu inayohifadhiwa. Alisema kuwa hatua hiyo imeongeza kipato kwa wananchi na hivyo kuwa sehemu ya suluhisho la kutunza mazingira kupitia faida za moja kwa moja.
Pia alisisitiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu upandaji wa miti ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda, kivuli na mapambo, akisema kuwa TFS imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza agizo hilo kwa vitendo.
“Rais alisema hataki kuona watu wakipanda miti ya ‘kizungu tu’ ya mapambo isiyo na tija kwa wananchi. Leo TFS wanapanda miti ya matunda, kivuli na hata ya mbao. Hii ndiyo maana ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi,” alisisitiza.
Aidha, Dkt. Timbuka alipongeza TFS kwa kutoa gawio kwa Serikali licha ya kuendelea na jukumu la msingi la uhifadhi wa mazingira. Alisema kuwa hatua hiyo inadhihirisha kuwa ni sahihi kutafuta vyanzo vya mapato visivyoharibu misitu badala ya kutegemea biashara ya mkaa na mbao pekee.
“Kama tunataka gawio kubwa bila kufikiria njia mbadala, tutaangukia kuruhusu ukataji wa miti hovyo. TFS wanatuonyesha kuwa inawezekana kupata mapato kupitia utalii wa Mazingira, asali na huduma nyingine rafiki kwa mazingira,” alisema.
Kwa upande wa utalii wa kiikolojia, Dkt. Timbuka alisema Wilaya ya Siha imeanza kunufaika na mikakati ya TFS kwa kuwa ni lango kuu la kuingia Mlima Kilimanjaro kupitia West Kilimanjaro. Alieleza kuwa maeneo hayo ni muhimu kwa wageni wanaohitaji siku za kujiandaa kabla ya kupanda mlima, hivyo uwekezaji wa huduma za malazi na mahema ni kichocheo muhimu cha pato la Taifa na mapato ya wakala.
“TFS wameleta mahema ya kisasa kwa wageni, sisi jukumu letu ni kuwasaidia kupiga debe kwa tour operators ili wafahamu huduma hizi zipo. Mapato haya yataongeza gawio na kutuwezesha kutoa huduma kwa wananchi kama Serikali,” alisema.
Akitoa salamu za Bodi ya Wadhamini wa TFS, Mjumbe Dkt. Siima Bakengesa alisema bodi hiyo hufanya ziara mara mbili kwa mwaka ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa majukumu ya wakala unakwenda kwa mujibu wa mipango na vipaumbele vya Serikali.
Dkt. Bakengesa alisema Wilaya ya Siha ni miongoni mwa maeneo yenye mafanikio ya kipekee katika usimamizi wa misitu, upandaji miti na uvumbuzi wa mbinu mpya za kuendeleza uhifadhi unaowanufaisha wananchi.
“Leo tumekuja Siha kujionea kazi zinazofanyika. Tunapokea maoni, changamoto na mafanikio, ili bodi irejee kuyafanyia kazi kisera na kimkakati. Tunafarijika kuona kuwa pamoja na kuhifadhi, TFS pia inachangia mapato ya Serikali na wananchi,” alisema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...