Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MASHILI COMPANY LIMITED ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Uchenjuaji Dhahabu wa (Matinje Mining, Msilale Mining na Igurubi Mining) Ndg Peter Andrea Mashili ametangaza nia ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini akiahidi kumg'oa Mbunge aliyepo Mhe Hussein Bashe ambaye ni Waziri wa Kilimo kwa madai kwamba anastahili kupumzika baada ya kuwatumikia wananchi katika kipindi cha miaka kumi.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nzega, Peter Mashili amesema kuwa ameamua Kugombea Ubunge kwa sababu wananchi wa Nzega wanahitaji nguvu na kasi Mpya ili kuendeleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025-2030.

Amesema akiteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kwenye mchakato wa kura za maoni na baadaye akiteuliwa kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Nzega Mjini atajikita zaidi katika ushirikishwaji wa wananchi kwenye mambo ya msingi ya maendeleo endelevu, kuwasemea wananchi Changamoto zinaowakabili, kuwapambania ili wanufaike na Fursa zinazotolewa na Serikali hasa katika uendelevu wa sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kwa lengo la Kukuza kipato kwa wananchi ili wajiendeleze kiuchumi na kukuza pato la Taifa.

Peter Mashili ambaye ni mbobezi katika uchimbaji na uuzaji wa madini ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mbugani katika Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora, ni miongoni mwa wafanyabiashara mahiri kuwahi kutokea nchini Tanzania ambao wana historia kubwa katika ushiriki wa shughuli za kijamii hususani uboreshaji wa miundombinu ya elimu.

Lakini wadadisi wa masuala ya kisiasa katika Jimbo la Nzega wanasema MASHILI wakati wake umefika sasa wa kugombea ubunge wa Jimbo hilo kutokana na kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wa wilaya ya Nzega kwa miaka mingi iliyopita na hadi Sasa bado anaendelea kufanya hivyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...